HADITHI; NAKUPENDA MADAM; Sehemu ya Tatu (3)

Tokeo la picha la PICHA ZA WAREMBO


TITLE: NAKUPENDA MADAM
SEHEMU ya Tatu.
Ilipoishia kipindi kilichopita...
Magdalena, taratibu machozi yalimtoka akamuangalia John naye machozi yalimtoka, akainuka na kumfuata mwalimu Magdalena akaanza kumfuta machozi.
Wakati mwalimu Magdalena anasimama ili amshukuru John kwa kumkumbatia, baba yake John anamuona akifanya hivyo, anakasirishwa na jambo hilo anawasogelea. sasa endelea
“Huo ndio ualimu wenye weledi, nauliza huo ndiyo weledi, nyie walimu wasichana kwa nini hivi, ni matatizo haujaolewa wewe, umeletwa huku kutufundishia watoto wetu ama kuwaharibu,’’ alifoka mzee Katuba baba wa John.“Mzee kukumbatia si vitu vya kawaida kuna jambo la kusikitisha kanihadithia John nikamkumbatia kwa kumfariji kwani kuna tatizo,’’ alijibu mwalimu Magdalena kwa kusitasita huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka machoni mwake.
“Nimesema mambo yenu ya kizungu huko huko mjini kwenu, huku kwetu hatutaki upuuzi wenu kama mmekuja kufundisha mfanye kazi ya kufundisha siyo kuharibu watoto wetu na we John haya ndani haraka,’’ akafoka na kumtaka John aingie ndani.
Mwalimu Magdalena akaondoka kwa haraka akikwepa kelele za mzee Katuba, aliyekuwa akimfokea huku akimfuata.
Hakuwa na furaha, mwalimu Magdalena aliingia na wasiwasi kwamba huenda hali hiyo ikamharibia kazi yake kijijini hapo, lakini licha ya hofu hiyo akajikuta akifarijika kutokana na kufutwa machozi na John mwanafunzi aliyempenda.
Alipofikiria jambo hilo nuru ya uso wake ikawa inarudi mvuto wake ukaangaza upya kama hakuwa na majonzi, aliruka huku na huko akifurahia siku hiyo kwani alishasahau yote yaliyomtokea kabla.
Akiwa njiani wakati huo wa usiku akipita kwenye njia nyembamba iliyokuwa na majani mengi huku pembeni kukiwa na mahindi yaliyokauka akaanza kuhisi kitu, kwani muonekano wake ukaanza kubadilika tena, alihisi anaona vitu ambavyo hakuvitambua vilikuwa vikitokea mbele yake na vingine vilikuwa vikitokea katika shamba la mahindi vikimfuata.
Giza lililotanda eneo hilo liliongeza vitisho kwa mwalimu Magdalena, kwa haraka akatambua kwamba huenda ikatokea tatizo eneo hilo, akaanza kujihadhari akavua viatu virefu alivyokuwa amevaa akavishika mkononi kisha akavuta nguo yake ndefu na kuishika mkono mmoja akaanza kutembea kwa tahadhari.
“Si nimekubamba ulifikiri utakimbia hadi lini,?’’ Sauti ilisikika lakini mtu hakuonekana, mwalimu Magdalena alishindwa kuendelea mbele akarudi nyuma huku mapigo ya moyo wake yakidunda kwa haraka.
Sauti na kitu kilivyoonekana kama sisira kilizidi kumfuata alivyokuwa akirudi nyuma alikotoka huku akiwatazama, kilichosikika hapo ni kicheko cha kejeli na sauti na woga aliyokuwa akiitoa mwalimu Magdalena.
“Nisaidieni nakufaaaa’ kwa haraka mwalimu Magdalena aligeuka na kukimbia huku akipiga kelele huku lile alilodhani kuwa ni sisira likizidi kumfuata na sasa likaonekana kuwa ni mtu alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike.
Lakini kabla hajafika mbali ghafla mwalimu Magdalena akakamatwa na kufumbwa mdomo, sauti haikusikika tena, alihangaika kujitoa katika mkono huo lakini hakuweza alijitupa huku na huko lakini mkono hule ulimshika vema ili sauti isitoke.
Itaendelea. Je, mwalimu Magdalena anafukuzwa na nani na nani aliyemkamata na kumfumba mdomo asipige kelele, usikose kufuatilia.

Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment