Mohammed Dewji /Mo ni nani
MO ni nani? Jibu; ni mfanyabiashara tajiri. Historia ya utajiri wake haina utata kusema labda aliwazidi ujanja nyakati za utafutaji, kwa hiyo wanamteka ili kulipa kisasi. Mo ni mtoto wa kishua mwenye akili. Alikuta mali nyumbani na kuziendeleza.
Jarida la Forbes Afrika liliandika mwaka 2013 kuwa Mo alikuta mtaji wa kama Sh50 bilioni mwaka 1998 kisha yeye akapiga kazi kisomi na kwa maarifa mengi hadi kufikia zaidi ya Sh3 trilioni ndani ya miaka 15.
Mo ni wa kishua. Alisoma Shule ya Msingi Arusha, sekondari akasoma Tanganyika International School. Mwaka 1992, alienda Marekani kusoma katika shule ya golfu ya Arnold Palmer, Florida kisha akasoma High School shule mbili za Florida, Trinity Preparatory na Saddle Brooke.
Alisoma Chuo Kikuu cha Georgetown, Washington DC, alikotunukiwa ganda lake la biashara za kimataifa na fedha. Mo pia amesoma dini. Aliwahi kusema alipomaliza chuo alijaribu kufanya kazi Marekani, kabla kuamua kurejea nchini ili kutumikia kampuni za familia yake.
Ni shabiki lialia wa Simba. Anaimiliki klabu hiyo kwa hisa asilimia 49. Juni 16, 2007, Taifa Stars iliipiga Burkina Faso nyumbani kwao bao 1-0. Mchezo ulikuwa wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2008.
Mo wakati huo akiwa mlezi wa Taifa Stars na mdhamini, aliungana na wachezaji kwenye gari la wazi, akawa kifua wazi pamoja na wachezaji. Hapa unajionea kuwa Mo ni tajiri msela, mtu wa kujichanganya. Zaidi, Mo aliwahi kuwa mmiliki wa Klabu ya African Lyon.
Mo ni mhisani. Ana mfuko wa kusaidia ustawi wa maisha ya Watanzania unaoitwa Mo Dewji Foundation. Katika tovuti ya mfuko huo, anasema: "Mungu anapokubariki kifedha, usinyanyue kiwango chako cha kuishi, nyanyua kiwango chako cha kutoa." Hapa unaona Mo si mbinafsi.
Si mbaguzi. Ungemuona gym akipiga picha na watu mbalimbali wa kawaida. Tabasamu lake lipo karibu. Mchangamfu. Ni mtu ambaye kila mmoja angependa awe rafiki yake. Wanaohoji kwa nini hatembei na ulinzi mkubwa, alishawapa jibu kabla hajatekwa, kwamba; ukibarikiwa fedha usijikweze, saidia wengine.
HISTORIA KAMILI YA MO DEWJI

0 Comments:
Post a Comment