HADITHI; NAKUPENDA MADAM; Sehemu ya pili ...........(2)

Tokeo la picha la PICHA ZA WAREMBO
TITLE: NAKUPENDA MADAM
SEHEMU ya pili.
 SAUTI ya kilio cha mwalimu Magdalena ilimshtua John, akakimbia mlangoni katika nyumba ya mwalimu akaanza kugonga ili kumtuliza mwenyekiti asitekeleze anachotaka kwa mwalimu Magdalena.
“N” aliendelea kuita mwalimu Magdalena huku mlango ukizidi kugongwa na kusababisha hali ndani ya chumba cha mwalimu huyo kuwa kimya
“Sasa ole wako umwambie mimi nipo humu ndani, kaongee naye umwambie hakuna kilichotokea bali ulikuwa unakumbuka kifo cha ndugu yako ndiyo maana unalia,’’ alitishia  mwenyekiti akimtaka mwalimu Magdalena akafungue mlango na kuzungumza na mtu aliyepo hapo wakati akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda.
Mwalimu Magdalena alikimbia kwa haraka huku akiwa ameshika kanga yake kifuani, hakujali namna alivyokuwa akionekana kutokana na kuwa na kanga moja aliyoifunga juu ya matiti yake yenye ushawishi mkubwa kwa wanaume.
Alipofungua mlango hakukutana na mwingine zaidi ya mwanafunzi John ambaye anampenda sana na ndiye aliyemsababishia hadi mwenyekiti amkute akiwa katika nguo moja.
‘Mwalimu nimesikia kila kitu, hivi kweli kwa kuwa nimekataa ndiyo uingize mwanaume mwingine, sijakudhania mwalimu kumbe una tabia za kishenzi hivyo,’’ John alimweleza mwalimu Magdalena aliyekuwa akimwangalia bila kujibu, roho ilimuuma akashindwa kujibu lolote zaidi ya kutoka machozi.
John hakujali machozi ya mwalimu Magdalena, aliondoka kwa haraka huku akimrushia maneno machafu mwalimu wake huyo aliyeonekana kuzidi kuingiwa na huzuni, kwani alifikiria kurudi ndani angekutana na mwenyekiti aliyekuwa na uchu wa kumbaka na mwanafunzi aliyekuwa akimpenda ndiyo hivyo amemjibu hovyo.
Mwalimu Magdalena alijifikiria kwa zaidi ya dakika 10 akajikuta akiishiwa nguvu taratibu aliposimama katika mlango akakaa chini kwa hasira alizokuwanazo machozi yalizidi kumtoka.
Mwenyekiti aliita kwa jazba akimtaka mwalimu Magdalena arudi ndani ili atimize alichokusudia, lakini kila sauti ya ukali ya mwenyekiti ilipomwita mwalimu Magdalena akajikuta akiingiwa na ujasiri akasimama na kumtaka mwenyekiti atoke nje ya chumba chake.
“Mwenyekiti nimekuvumilia vya kutosha, nimekuheshimu vya kutosha na pia umenidhalilisha vya kutosha, naomba utoke kwangu kabla sijafanya maamuzi magumu tokaaaa…’’ alifoka mwalimu Magdalena huku akikifuata kilipo kisu
Sauti hiyo ilimtisha mwenyekiti, hakufikiria kama mwalimu huyo angeweza kubadilika, hivyo aliiangalia sura ya mwalimu Magdalena ilikuwa ikibadilika taratibu, tabasamu lake lilianza kupotea ndita zikaanza kujitokeza, mikono yake iliyokuwa imeshika kisu ilianza kutetemeka kiasi cha kumtisha mwenyekiti, kwa haraka akavuta shati lake lililokuwa juu ya kitanda cha mwalimu Magdalena akaliweka begani na kutoka kwa haraka.
“Naondoka lakini na wewe jiandae kuondoka, siwezi kukaa na aibu lazima nawe uondoke kijijini kwangu mi ndiyo mwenyekiti,’’ alijinadi mwenyekiti huku akiwa ameshika mlango tayari kwa kuondoka, mwalimu Magdalena hakujibu kitu zaidi ya kumuangalia kwa sura ya ukali.
Mwenyekiti alipotoka hali ya mwalimu Magdalena ilirudi taratibu lakini mawazo yake yote yalielekea kwa mwanafunzi John, alifikiria namna ya kumpata kabla haijafika siku ya pili na akaanza kusambaza taarifa zake ambazo hazikuwa za kweli.
Kwa haraka akavaa nguo zake akatoka na kwenda nyumbani kwa John, hakujali muda alitembea kwa umbali gani wala alikutana na nani, alichokuwa akikifikiria ni kukutana na John na kuzungumza naye ili tofauti zao ziwe katika muafaka.
Alifika karibu na nyumba ya kina John akatumia nafasi yake ya ualimu akamuomba John wakasogea karibu ya nyumba yao na kuzungumza.
“John sikiliza wewe siyo mtoto kihivyo, unavyonifanyia sijapenda mimi ni binadamu naumia au kwa kuwa nimekuonyesha nakupenda,’’ alijieleza mwalimu Magdalena lakini John alikuwa kimya
“Nazungumza nawe John mbona hata haunijibu kwa nini hivyo, sikiliza mimi sikufanya chochote na mwenyekiti wala sikumuita wakati ulipoondoka ghafla nikasikia mlango ukifunguliwa na unajua uliniacha nikiwa katika mazingira gani hivyo nikajua kwamba ni wewe umerudi na giza la ndani sikuweza kuona nilidhani wewe John lakini sauti na mikono iliponigusa nikagundua siyo wewe kumbe alikuwa mwenyekiti ameingia akitaka kunibaka na pale ulipokuja kugonga ukawa umenisaidia asiweze kutimiza azma yake, nashukuru kwa kurudi tena lakini kama utanifikiria vibaya Mungu anajua, ninakuhakikishia sikufanya lolote na mwenyekiti,’’ anasema mwalimu Magdalena, taratibu machozi yalimtoka akamuangalia John naye machozi yalimtoka, akainuka na kumfuata mwalimu Magdalena akaanza kumfuta machozi.
Wakati mwalimu Magdalena anasimama ili amshukuru John kwa kumkumbatia, baba yake John anamuona akifanya hivyo, anakasirishwa na jambo hilo anawasogelea.
Nini kitaendelea, hivi baba yake John atafanya nini? je,watakachomweleza atakielewa? na vipi kuhusu mwenyekiti atafanikiwa niya yake ya kumwondoa kijijni mwalimu magdalenae.itandelea usikose... 
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment