Ilipoishia
Mwalimu Magdalena alikimbia huku
akipiga kelele bila kujua anakokimbilia angepata msaada ama la! Alishaanza
kuchoka na ilikuwa giza sana, lakini alichoambulia kugundua ni kwamba mtu
aliyekuwa akimkimbiza alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike. Sasa Endelea
GHAFLA mwalimu
Magdalena akajikuta akikamatwa na kufumbwa mdomo, alikukuruka ili ajitoe katika
mikono iliyombana vema, lakini hakuweza kuitoa, alijitahidi kujitoa mbele ya
mtu huyo aliyemfumba mdomo, sauti pia miguu yake havikumsaidia kufanya chochote
kujikwamua kutoka eneo hilo.Mwenyekiti alishangaa
kutosikia sauti ya mwalimu Magdalena, akaangaza huku na kule, lakini hakuweza
kutambua wapi alipo mwalimu Magdalena, alinyanyua macho huku na huko, lakini
hakufanikiwa.
Taratibu Mwalimu
Magdalena alikuwa akipoteza nguvu kutokana na kubanwa na asiyemjua, mtu yule
alimvuta eneo lingine ili kumkwepa mwenyekiti aliyekuwa akimsaka mwalimu
Magdalena ili atimize ahadi yake.
Mwenyekiti alianza
kuhamaki alipojificha mwalimu Magdalena, akavua kinyago alichokivaa kuficha uso
wake, akaingia katika majani anayohisi mwalimu Magdalena amefichwa.
Mwenyekiti alikanyaga
majani yale akiamini mwalimu Magdalena amejificha na yupo peke yake, akazidi
kusogea ghafla, naye akashtukia amekabwa na kitu asichokijua.
Mwenyekiti alipiga
kelele huku akijitahidi kutoa mkono uliomkaba, lakini hakuweza, akatumia akili
za kuruka sarakasi na kujidondosha huku na huko, akapata nafasi ya kujinasua
katika mkono huo, hakuwa na ulazima wa kupambana na mtu asiyemjua, akaamua
kutimua mbio.
Mwalimu Magdalena taratibu
akanyanyuka na kutaka kukimbia, lakini yule mtu aliyemkamata na kumziba mdomo
akamkamata kisha akajitambulisha kwake.
“Sitaki, sitaki, sitaki
mwenyekiti,’’
“Mwenyekiti, mwenyekiti
ndiyo nani mi siyo mwenyekiti, nimekusaidia ulikuwa katika hatari nimekuokoa,’’
walishindwa kuelewana kutokana na giza lililotanda siku hiyo, mwalimu Magdalena
alianza kupunguza woga lakini hakutambua sura ya mtu huyo aliyemweleza kuwamba
amemuokoa.
Alijitahidi kumtazama
lakini hakuweza, mtu huyo alitambua kwamba mwalimu Magdalena anataka kumtambua
ni nani, akaingiza mkono wake mfukoni kwake akatoka na simu akawasha tochi kisha
akajimulika usoni na kumtaka mwalimu Magdalena amwangalie.
“Wewe ni nani? Umesema
ni mwalimu, mwalimu gani na huku umefuata nini?’’ alihoji.
“Mimi ni mwalimu Jokam,
wengi wanapenda kuniita Joka.’’
“Joka’’ alihoji kwa
hofu mwalimu Magadalena.
“Ndiyo ni Joka kwa kuwa
ni mtaalamu wa hisabati, huwa sishindwi chochote katika hisabati na nililetwa
kijiji hiki muda mrefu lakini sikupenda lakini kuna jamaa yangu aliniambia
aliwahi kufika huku na kuna fursa nyingi huku ndiyo nimekuja kuangalia kama ni
kweli nije kufanya kazi huku.’’ Alifafanua mwalimu Joka.
“Tatizo ni nini hadi huyu
mwenyekiti akukimbize hivyo.’’
“We acha tu ni story
ndefu.’’
“Nisimulie nitakusaidia.’’
“Najua utanisaidia, ila
turudi kwanza nyumbani kisha kesho asubuhi nitakuhadithia kama unataka.’’
“Sawa ila mimi ni
mwenyeji wa mwenyekiti.’’
“Sasa mwenyekiti
mwenyewe ndiyo huyo umemtimua.’’
“Kazi ipo kweli kweli
sasa nifanyeje?’’
“Twende kwangu mambo
mengine yote utajua asubuhi, maana ni usiku na umenisaidia sana kuniokoa, ila
mimi sihitaji hata fursa zilizopo, kesho mapema nitaanza safari ya kurudi
mkoani kwetu bora nikawe mama wa nyumbani huko kuliko kuteseka hapa na
mwenyekiti,’’ alilalama mwalimu Magdalena.
“Ahaaa! Huyu mwenyekiti
ndiyo akusumbue wewe nitadeal naye we niachie mimi tena nitamweka wazi kwa watu
wote, kwani hana mke.’’
“Hata sijui,’’ alijibu
mwalimu Magdalena.
Mazungumzo yao
yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi,
kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta
wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona
mwalimu Magdalena shuleni.
“Sasa itakuwaje, nje
kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona
itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa
naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.’’
“Sawa.”
Unadhani nini kitaendelea hapo ikitokea John akibaini kuwa mwalimu magdalena yuko ndani. usiko kipindi kijacho.....
0 Comments:
Post a Comment