ilipoishia
Mazungumzo yao
yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi,
kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta
wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona
mwalimu Magdalena shuleni.
“Sasa itakuwaje, nje
kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona
itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa
naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.’’
“Sawa.” sasa endelea
Mwalimu Magdalena
alipotoka nje akakutana na John, mwanafunzi anayempenda, John hakutaka kuhoji
chochote hadi aingie ndani lakini mwalimu Magdalena alionyesha hofu kama ya
kusita, lakini akakubaliana na yote, John akaingia akakaa kitandani huku mwalimu
Joka akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda cha mwalimu Magdalena.
“Mwalimu mbona hadi
sasa hujafika shuleni kila mtu anahofu nawe, hakuna anayeelewa somo lolote hadi
wakuone, mwalimu unanujua wanafunzi wa shule ile tulivyokuzoea na pia kuna taarifa
kwamba mwenyekiti alikubaka jana ni kweli mwalimu Magdalena,’’ alihoji John
huku uso wake ukionyesha kukasirishwa na kitendo hicho.
“Hapana John hakunibaka,
ni kweli lengo lake lilikuwa hilo maana alinikimbiza kichakani usiku mzito
lakini alishindwa kufanikiwa.’’
“Alishindwaje wakati
mlikuwa wawili? Mi nilijua mwalimu Magdalena huwezi kusubiri unaona sasa,
mwenyekiti namchukia maisha yote,’’ alilalama mwanafunzi John huku mwalimu
Madgalena akibubujikwa namachozi akishangaa nani katangaza habari hizo
akatambua kwamba atakuwa ni mwenyekiti.
“John hapana
hakufanikiwa kufanya hicho kitendo ingawa alinikimbiza lakini niliokolewa na
mtu mwingine huko msituni alimpiga mwenyekiti akakimbia mimi bado nipo vizuri
na nakusubiri John wangu usiwe na hofu,’’ alijibu mwalimu Mgadalena huku wote
wawili John na mwalimu Mgdalena wakitokwa na machozi.
Walifutana machozi pale
wakajikuta nao wakipitiwa na usingizi. Muda ulipita walipokuja kusituka ilikuwa
jioni.
John alistuka kuona
muda umekwenda hivyo kwa haraka akaelekea kwao akimwacha mwalimu Magdalena
ajiandae kujibu maswali kuhusu John.
Lakini alipoita hakuna
aliyeitika na alipochungulia uvunguni hakumuona mwalimu Joka, akashangaa kwa
nini hakumuona, alijiuliza maswali mengi asijue alipoelekea mwalimu huyo lakini
akili ilimtuma kuamini kwamba mwalimu huyo alitoka wakiwa wamepitiwa na
usingizi na John.
Jioni ya saa 12
Mwalimu Joka alifika kwa mwenyekiti na
kujitambulisha kwamba yeye ni mwalimu aliyetakiwa kufika katika kijiji hicho kusaidia
kuokoa somo la hisabati lililokuwa likielekea kupotea kwa kuwa hakuna
mwanafunzi aliyekuwa akilipenda somo hilo kutokana na kutokuwa na mwalimu wa
somo hilo kwa miaka mingi zaidi ya wanafunzi wa kujitolea ambao walifika
kijijini hapo kwa mafunzo.
Mwenyekiti alionyesha
kutofurahishwa na mwalimu huyo aliyekuwa na umbo la wastani lenye nuru angavu,
sura yenye mvuto.
Hofu ya mwenyetiki ni
kwamba ujio wa mwalimu huyo ni pigo kwake kumfuatilia mwalimu Magdalena kwa
kuwa tayari atapata mlinzi na kwa vyovyote watapendana kwa kuwa wote wametoka
mjini, hivyo watakuwa wanapenda maisha yao yaendelee.
Nini kitaendelea hadi kipindi kijacho. Je, mwalimu Magdalena na Mwalimu Joka wakikutana watazungumza nini na
je, mwenyekiti atagundua kwamba mgeni wake ndiye aliyemkimbiza porini. Usikose
kufuatilia.
0 Comments:
Post a Comment