HADITHI; NAKUPENDA MADAM; Sehem ya Sita ..........(6)


Tokeo la picha la PICHA ZA WAREMBO
Ilipoishia wiki iliyopita
MWALIMU mpya kijijini hapo, Mwalimu Jokam (Joka) amefika kwa mwenyekiti bila kujulikana kama ndiye aliyemsaidia Mwalimu Magdalena asipate madhara kwa mwenyekiti wa kijiji hicho.


Mwalimu Magdalena naye anajikuta akiwa katika wakati mgumu kwani baada ya kupitiwa na usingizi alipokuwa na mwanafunzi John, mgeni wake aliyekuwa amemficha chini ya uvungu wa kitanda chake alishindwa kuvumilia akaamua kuondoka na leo kwa mara ya kwanza wanakutana wakiwa darasani, 
Sasa endelea kufuatilia hadithi hii ya kusisimua ya Mwalimu Magdalena.



Katika hali isiyotarajiwa wakati mwalimu Magdalena akimaliza kipindi chake cha historia kipindi kilichofuata ni hisabati, kilichofuata hapo ni hali ya mshangao uliotoka kwa mwalimu Magdalena.
Kitendo cha mwalimu Magdalena kumuangalia kwa muda mrefu mwalimu Joka kilitafsiriwa tofauti na John, lakini hakikuleta fikra tofauti kwa kuwa imani ya wanafunzi ni kwamba walimu hao ndiyo kwanza walikutana.


Haikuwezekana kunyamaza kimya licha ya mwalimu Joka kuonyesha kuchukizwa na jambo, lakini hakuweza kutoitikia salamu ya mwalimu Magdalena.


“Mwalimu Joka ndiyo umefika? Maana sikukuoana ofisini asubuhi,” aliuliza Mwalimu Magdalena.



“Hapana nilikuwepo,” alijibu kwa mkato mwalimu Joka, sauti iliyotumika kujibu hilo swali ilimuonyesha dhahiri kwamba amekasirika hivyo mwalimu Magdalena alihama kuondoka darasani na kumuachia aendelee na kipindi chake.


“Sawa naomba ukimaliza kipindi tuzungumze jambo kidogo”
“Sawa” alijibu huku akielekea mbele ya dawati lililowekwa mbele kama meza ya mwalimu wa kipindi na kisha akajitambulisha kwa wanafunzi hao kwamba, yeye ni mwalimu wa kipindi cha hisabati huku akiwaasa wafuate anachowaelekeza ili waweze kulipenda somo hilo.



Mtihani ulibaki kwa mwalimu Magdalena alikwenda moja kwa moja hadi ofisi ya walimu, alisogea kwenye kiti chake akatulia kimya bila kuanzisha mada wala kuchangia chochote kilichokuwa kikijadiliwa na walimu wenzake katika ofisi hiyo.


Mazungumzo ya chini kwa chini yaliendelea katika chumba hicho cha walimu, wapo waliodhani kwamba mwalimu Magdalena ametulia kimya kutokana na kashfa iliyozagaa ya kubakwa na mwenyekiti wa kijiji hicho lakini pia wapo waliodai mambo mengine lakini kilichokuwa kikimuumiza kilikuwa moyoni mwake.



“Najua kanikasirikia kwa sababu ya John, hakuna lingine ni hilo tu maana wanaume kunisaidia siku zile keshachukulia ‘advantage any way’ lakini nisimzungumzie inawezekana amekasirishwa na yake ngoja atoke nizungumze naye nitajua,’’ alijisemea mwalimu Magdalena huku akiwa anapitia daftari la mahudhurio ya wanafunzi lililokuwa mezani kwake.
“Ndiyo mwalimu Magdalena, nimeitikia wito,” alikuwa mwalimu Joka baada ya kutoka darasani alifika kwa mwalimu Magdalena kama alivyomtaka afanye hivyo baada ya kipindi chake.
“Nashukuru umekuja lakini hatuwezi kuzungumza hapa ofisini twende nje.”
“Nje tena, mi sitaki mambo ya kitoto maana nasikia una mpenzi mtoto wa hapa shuleni.’’
“Hayo ya nini Joka, hayo maisha yangu nataka tuzungumze mambo mengine hayo niachie mwenyewe nitamaliza.”
“Na ya Mwenyekiti, utayamaliza vipi na kubakwa kwako.”
“Joka usinifedheheshe, unajua ukweli wote wa mwenyekiti lakini kama umeamua kuniharibia sikukatazi unaweza kufanya hivyo maana wewe ndiye unayejua ukweli wa tukio zima la usiku ule,” alijieleza mwalimu Magdalena akimtazama mwalimu Joka akiwa amesimama mbele ya meza yake ndani ya ofisi ya walimu.
Walizungumza mengi wakafikia mwafaka wa kwenda kuzungumza nje ya ofisi hiyo, lakini wakiwa katika harakati za kutoka ofisini hapo, wanasikia kelele kutoka nje ya ofisi huku wanafunzi wa madarasa mbalimbali wakitoka darasani.



Walimu nao wakashangazwa na tukio hilo wakachungulia nje kuona kwanini wanafunzi walikuwa wakitoka nje ya madarasa yao na kukimbilia nje.
Akiwemo mwalimu Magdalena na Joka walichokiona hawakuamini kwani alikuwa baba wa John aliyekuwa akimchapa John bakora huku akimtaka akamuonyeshe mwalimu Magdalena.
Mwalimu Magdalena alifedheheka hakuweza kutoka nje ya ofisi, alijisikia vibaya kumsikia mzee huyo aliyeonyesha kukasirika akiwa na bakora mkononi akimtaja jina lake huku akirusha baadhi ya maneno ya kufedhehesha.


Wanafunzi walizidi kushangilia kila mzee huyo alipomcharaza bakora mwanaye huku akimtaka kuzingatia masomo badala ya mwalimu Magdalena.



Haikuwa siri tena kila aliyekuwepo katika eneo hilo alisikia kila kitu kilichokuwa kikizungumzwa na baba huyo wa John, maneno makali na yasiyosimulika yalimuumiza Joka akamtazama mwalimu Mgdalena aliyekuwa ameanza kutokwa na machozi akiwa amejiinamia katika meza yake ofisi ya walimu akaingiwa na huruma.



Akatoka moja kwa moja hadi kwa mzee huyo akamtaka wakazungumze katika ofisi ya mwalimu mkuu, mzee huyo akaleta mzozo 
Je baba yake john atazua mzozo gani, je atakubali kwenda ofisini?,Aibu kwa mwalimu Magdalena ataficha wapi uso wake jambo hili likifika kwa mwalimu mkuu? USIKOSE SEHEMU YA 7 
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment