HADITHI; NAKUPENDA MADAM; Sehem ya Saba................(7)

Tokeo la picha la PICHA ZA WAREMBO
Ilipoishia kipindi kilichopita
 Haikuwa siri tena kila aliyekuwepo katika eneo hilo alisikia kila kitu kilichokuwa kikizungumzwa na baba huyo wa John, maneno makali na yasiyosimulika yalimuumiza Joka akamtazama mwalimu Mgdalena aliyekuwa ameanza kutokwa na machozi akiwa amejiinamia katika meza yake ofisi ya walimu akaingiwa na huruma.



Akatoka moja kwa moja hadi kwa mzee huyo akamtaka wakazungumze katika ofisi ya mwalimu mkuu, mzee huyo akaleta mzozo sasa   endelea
 kisha akakubaliana na kauli ya mwalimu Joka



“Mzee hapa si sehemu sahihi ya kueleza kero yako mi nakuomba mzee wangu twende ofisi ya mwalimu mkuu kule tutazungumze na kukusikiliza vizuri, lakini kusimama hapa tutaendelea kujifedhehesha.’’
“Nakubali kwa kuwa ni mwanaume umenieleza maneno hayo, ila nakwenda huko nataka mumuite na huyo mwalimu nimkanye kwa mara nyingine maana mara ya kwanza alikuja nyumbani kwangu leo amelala na mwanangu siku nzima anarudi usiku,’’ alilalama kwa sauti mzee huyo na kuwaacha na mshangao wote waliomzunguka wakiwemo baadhi ya walimu wa kike.


Mwalimu Joka akampeleka mzee huyo hadi ofisi ya mwalimu mkuu lakini mwalimu mkuu hakuwemo wala msaidizi wake, ikabidi achukue jukumu la kuzungumza na kumskiliza kero zake kwa niaba ya mwalimu mkuu.



“Mzee wangu nakusikiliza nieleze kila kitu kuhusiana na kero yako,’’ alitaka aelezwe mwalimu Joka huku mzee huyo akiwa amekaa kwenye benchi akiwa na John.



Alianza kujieleza; “nisichopenda ni kwamba sitaki tabia hii ya kishenzi ya mwaimu wenu kumharibu mtoto wangu, mwanzoni alimfuata nyumbani kwangu akaona haitoshi juzi akamchukua mtoto wangu akaenda kulala naye huyu mwanafunzi atalalaje naye, isitoshe yeye ni mtu mzima huyu bado mtoto mdogo anamuingiza katika mapenzi walimu wenzake hawamtoshi nimesema sijapendezwa na tabia hii, nataka aje hapa nimkanye,’’ alieleza kwa ukali mzee huyo.



“Usijali mzee wangu kwa bahati mbaya mwalimu mwenyewe alikwisha ondoka maana alikuja shuleni akafundisha kipindi kimoja, lakini akaaga kwamba anaumwa mi nikuahidi nitafikisha ujumbe huu kwake.


Na pia lazima tukutane kamati ya shule tujadili jambo hili kisha tutakuita na kukukutanisha na mwalimu huyu, ili aombe msamaha na kuachana na tabia hiyo mbaya kwa kweli hadi mimi nimefedheheshwa na tabia hiyo, tunawafundisha nini sasa hawa wanafunzi wetu,’’ alisisitiza mwalimu Joka.

Walizungumza mengi kisha John na baba yake wakaondoka kurudi nyumbani kwao, wakati hayo yakiendelea mwalimu Joka kwa haraka alirudi ofisini kwa walimu ili azungumze na mwalimu Magdaena, lakini hakumuona na alipohoji walimu wengine wakasema kwamba alikwishaondoka kutokana na aibu hiyo.
Mwalimu Joka alishagundua mazingira na mawazo ya walimu wenzake waliokuwa ofisini humo, hakuweza kueleza chochote katika mazingira yale hakusubiri ruhusa ya yoyote akatka nje ya ofisi na kwenda nyumbani kwa mwalimu Magdalena.
Alipofika aligonga mlango na mwalimu Magdalena akaenda kuufungua akaingia ndani, lakini ghafla akajikuta akishangaa kumuona John akiwa amekaa kitandani bila wasiwasi wowote.


Nini atafanya mwalimu Joka baada ya kumkuta John kitandani kwa mwalimu Magdalena. 
Itaendelea wiki ijayo iwapo tu itapata like za kutosha kutoka kwenu kwani mwendelezo wake unatokana na mapokeo yenu
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment