CHIMBUKO LA UGONJWA WA UKIMWI DUNIANI

  FREEDOMLEO BLOG


  Ugonjwa wa ukimwi ni ukosefu wa kinga mwilini baada ya virusi aina ya lentivirus kushambulia chembe chembe  nyeupe za damu zenye uwezo wa kuukinga mwili usishambuliwe na magonjwa mbalimbali.
  Ugonjwa huu  umegundulika  katika karne 19 na 20 baada ya virusi aina ya simian immunodeficiency virus (Siv)kutoka kwa wanyama aina ya Sokwe na kwenda kwa binadamu na kubadilika kuwa human immunodeficiency  virus(HIV) huko jangwa la Sahara huku ukigawanyika katika makundi makuu mawili HIV-1 NA HIV2.
  HIV-1 iligundulika kusini mwa Cameroon kutoka kwa sokwe hadi kwa binadamu na HIV2 imetokana na nyani waliofahamika kwa jina la  Sooty Mangabey ambao walikuwa wanapatikana Afrika  Magharibi na kusini mwa Senegal.
  Zipo nadharia mbalimbali zinazoelezea chanzo, chimbuko  na asili ya  ugonjwa huu wa ukimwi nazo ni,
                      1:NADHARIA YA UWINDAJI.
  Nadhari hii inaelezea kuwa ugonjwa wa ukimwi umetokana na virusi aina ya simian immenodiffiency virus(SIV) kuhamia kwa binadamu baada ya kula nyama mbichi ya sokwe waliowaua au damu kuingia kwenye vidonda vya  wawindaji hao ilionekana bara la Afrika kati ya miaka 1980.

                     2:NADHARIA YA KINGA YA POLIO.
 Inaelezea chimbuko la ukimwi kuwa ulianza kwenye majaribio ya chanjo ya polio iliyojulika kwa jina la CHAT iliyotolewa kwa watu takribani milioni moja wa CONGO,RUANDA na BURUNDI kati ya miaka 1950 huku ikisemekana ya kuwa chanjo hiyo ilikuzwa ndani ya seli za figo za sokwe walikuwa na virusi aina ya simian immenodifficieny  virus na kusababisha watu kupata  HIV-1.

                     3:NADHARIA YA SINDANO.
 Nadharia hii ni muendelezo wa nadharia ya uwindaji inasema ya kwamba katika miaka ya mwanzo ya 1950 sindano zilianza kutumika ingawa ilikuwa ni kwa mara chache sana katika nchi za Afrika huku wafanyakazi wa idara ya afya waliendelea kutumia sindano moja kwa watu wengi kutokana na hili suala inawezekana kuwa ilieneza virusi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

                    4:NADHARIA YA UKOLONI.
 Katika miaka ya mwanzo ya karne ya 19 na ya mwisho ya karne ya 20 ukoloni uliingia katika maeneo mbalimbali Afrika ikiwemo maeneo ya BELGIAN CONGO  na FRENCH EQUATORIAL AFRIKA ambapo watawala hawakuwathamini watu walio watawala kutokana na hali hii wa Afrika wengi walijikuta wakiwa kwenye makambi ambako hali ya usafi zilikuwa duni na chakula kilikuwa kichache kutokana na hali hiyo ili wapasa kula nyama za sokwe kutokana na afya zao kuwa duni virusi waliwashambulia kwa urahisi na kudungwa sindano zisizochemshwa.

                  5:NADHARIA YA UANGAMIZAJI.
 Nadharia hii inaelezea ya kwamba ukimwi ulitengenezwa nchini MAREKANI na shirika la US-FEDERAL SPECIAL CANCER VIRUS PROGRAM ikiwa ni njama ya kuua watu weusi na watu wanao shiriki mapenzi ya jinsia moja (mashoga) kote duniani.
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment