HISTORIA YA FREEMASON TANZANIA




                                   FREEDOMLEOBLOG


Sir Chande: Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi na alikutana na watu wengi ambao walikua wanahudhuria vikao vya freemasons, akaanza kuuliziaulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu hao watu. 
Kwa wakati huo, hao watu hawakua huru kuzungumzia Freemasons kama anavyofanya chande sasa hivi, haswa kabla ya vita ya pili ya dunia.
Sir Chande anasema wakati huo Freemasons ilikua imegawanywa kwenye makundi tofauti, katika mahospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikua na kundi maalum la freemasons kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa serikali, ukiangalia vizuri wengi wao walikua wazungu na baadhi ya wahindi.
Kundi la kwanza lilikua linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofata yalikua yanaongozwa na waingereza na kundi la nne lilikua linaongozwa na wahindi ambalo kundi la nne ndilo Chande alilojiunga nalo nalo, ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na freemason, aliapishwa rasmi rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28, kumbuka kwamba masharti ya kujiunga na freemasons ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.
Baada ya hapo ndipo alipoanza kupenda Freemasons ambapo pia alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la freemasons katika nchi nne ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda na sychels na akajiunga na miradi tofauti ya freemasons nchini uingereza yakiwemo mahoteli ya kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya freemasons nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari sana.
Hoteli nyingine ya kifahari alisimamia ujenzi wake iko Zambia.

FREEMASONS NI NINI?
Ni taasisi ambayo ilianzishwa miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi, wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua
.

Anasema “Freemasons sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya, Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”

NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA:
Kwa nchi za Afrika Freemasons imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja wetu.
 
Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.
 


KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada kwa watu wasio jiweza.



WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI:
Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.
 


JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS:

Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli .
Ni lazima Upende kutoka moyoni wewe kujiunga na freemasons na kuwa tayari kutoa misaada freemasons.

Unapotaka kujiunga ni lazima utume maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama hujui mtu unaandika barua au kuwasiliana na sir andy chande  kwa namba zake hapo chini ,baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia kwenye freemasons itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au mumeo au familia wakiwa kama rafiki.

Inaweza kuchukua mwaka mmoja na nusu au mwaka kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu, baada ya hapo ili uwe freemason kamili kuna vyeo vitatu ambavyo tunaviita degrees ambavyo ni lazima uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.


BAADA YA KUJIUNGA:
Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.
 

KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:
Acha nizungumzie Freemason ya Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.
Kazi zote zinazofanyika na Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya misaada mikubwa yanatoka Uingereza.
Kuna mahoteli ya freemasons Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.
Watu wengi huwa wanasema ni taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu, vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema tukifanya ibada zetu.
Kwa afrika Mashariki makao makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya kwa sababu aliechukua nafasi yangu yuko Nairobi na pia makamu wake yuko Nairobi, Kuna majumba 50 ya freemasons Afrika Mashariki
Ingawa makao makuu yako Nairobi, jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi yetu yanafanyika hapa hapa.
 


4385 - HAVEN OF PEACE LODGE
Consecrated 31st March, 1922
by R. W. Bro. Sir ANDY CHANDE. Bowring
FM Hall, DAR-ES-SALAAM
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment