Katika sayari hii ya dunia kuna baadhi ya watu wanakwambia mapenzi ndiyo
yanayoiendesha dunia, hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya watu wengi
wametawaliwa na mawazo ya kimapenzi.
Pamoja na kuwapo kwa
kundi hilo la watu wanaoamini hivyo lakini pia wapo baadhi ya watu
huamini ya kwamba mapenzi hayana faida yeyote ile.
Kundi hili
la watu hao hujikuta wakitoka kwenye mahusiano, na sababu
zinazopelepekea wao waamini hivyo mara nyingi huwa zinatokana na maumivu
ya kutendwa na mtu ambaye alikuwa anamuamini na leo hii hayupo na mtu
huyo tena kwenye mahusiano.
Tumekusogezea faida za kuwa single katika ulimwengu huu.
1. Mtu anapokuwa single anakuwa na uhuru wa muda wa kufanya mambo yako
binafsi pasipo kupelekeshwa na mtu yeyote yule. Uhuru huu wa muda ni ule
wa kufanya mambo yake na ya kijamii pia.
2. Mtu ambaye yupo
single unakuwa na uhuru pia wa kufanya kile inachokitaka/ anachokipenda.
Unapokuwa kwenye mahusiano kunakosekana uhuru wa kufanya vitu
uvipendavyo hii ni kwa sababu unaweza ukawa unapenda kufanya jambo
fulani ila kwa kuwa upo kwenye mahusiano ya kimapenzi huyo mpenzi wako
akakuzuia kufanya jambo hilo kwa kuwa jambo hilo halimpendezi.
3. Unapikuwa single unakuwa hauna hisia mpelekesho, hisia mpelekesho ni
zile hisia za kimapenzi ambazo zinakufanya ifikiri sana kuhusu mambo
yanayohusu mapenzi, kwa mfano hivi hujawahi ona mtu anakurupuka usiku wa
manane anampigia simu mpenziwe? bila shaka umewahi kuona, hii ni tabia
inayokwenda sambamba na kitu kinachoitwa wivu. Hivyo unapokuwa single
unakuwa hauna wivu kwa sababu unakuwa hauna mtu ambaye anakufanya uwe
hivyo.
4. Unapokuwa single hakuna lawama zinazohusu mahusiano
ambazo zitakuwa zinakuhusu wewe. Unapokuwa kwenye mahusiano yapo
malalamiko mengi ambayo yatakuwa upande wako, vitu kama kwanini hupokei
simu yangu na mambo mengine kama hayo yatakuwa mbali na wewe.
5. Utaishi maisha marefu yenye mjumuiko wa amani ya moyo pamoja usiokuwa na bugudha wala makwaluzano ya aina yeyote ile.
6. Kila siku Utalala usingizi mzuri.
7 Faida nyingine ya kuwa single utaongeza mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Comments:
Post a Comment