NAMNA YA KUANDIKA BARUA YAKUOMBA KAZI

Umeshawahi kupanik baada ya kujua kwamba inabidi uandike barua ya kuomba kazi?

Ingawa kutafuta ajira Tanzania ina changamoto zake kwa ujumla, kuandika barua la kuomba kazi ina ugumu wake pekee.  Ila, ni muhimu sana kuandaika barua ya kuomba kazi ukiwa unatafuta kazi, hata kama hulazimishwi kufanya hivyo.

Kwa nini ufanye kazi ya ziada?

Barua yako ya kuomba kazi ni nafasi yako ya kujiuza kwa mwajiri. Usirudie yaliyomo kwenye CV yako. Badala yake, elezea umefikaje hapo ulipo kwenye swala la kazi, pamoja na kuonyesha ujuzi uliyofanikiwa kupata mpaka hapo. Itasaidia kukutofautisha kwa mwajiri.

Zaidi ya kukumbana na ushindani mkubwa wa kutafuta ajira, hakuna lingine tunaloweza kufanya. Kwa kuandika barua ya kuomba kazi tunajiongezea nafasi ya kuajiriwa kwa mwajiri. Kwa hiyo ni muhimu sana kuweka muda maalum kuiandaa, kama vile unavyofanya kuandaa CV.

Kwa kuwa sisi ni rasilimali kubwa zaidi Tanzania kwa waajiri na wanotafuta ajira, tumejifunza vidokezo mbali mbali zitakazo kusaidia kuandika barua ya kuomba kazi itakayojitokeza vizuri. Zifuatayo ni vidokezo kumi bora vya kuandika barua ya kuomba kazi.

1. Utafiti

Hatua ya kwanza ya kuandika barua ya kuomba kazi ni kujua zaid kuhusu kampuni/shirika unaloomba kazi pamoja na hiyo nafasi ya kazi yenyewe.

Pitia tovuti ya kampuni pamoja na walipo kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, LinkedIn n.k). Jaribu kujua maadili ya kampuni yakoje, changamoto zake na jinsi gani utachangia kuiboresha kampuni hiyo. Kwa kujua haya yote, utaweza kuandika barua itakayo onyesha kwamba unawaelewa na ni jinsi gani utawasaidia.

Kwa mfano, kama unatafuta kazi kwenye shirika la ajira, fanya utafiti kujua kwamba kikwazo kimoja kikubwa kwa waajiri Tanzania ni kutafuta watu wenye sifa za kazi zinazowafaa. Kwenye barua yako unaweza kueleza ni jinsi gani ujuzi wako imekuandaa kutatua tatizo hili kwao.

Kumbuka, barua ya kuomba kazi ni njia yakumpa mwajiri maelezo ya kiundani zaidi juu yako wewe, sio tu kuorodhesha vitu amabavyo vilishaorodheshwa kwenye CV yako.

2. Tuma barua kwa mtu maalum

Maelezo ya kazi yanaweza yasiwe na jina la afisa wa rasilimali watu au Mkurugenzi Mtendaji, ila jitahidi kujua ni nani haswa atakayepoke maombi ya kazi.Hii inaweka uzito zaidi.

Utatafutaje jina la mhusika?

  • Itafute kampuni hiyo kwenye LinkedIn alafu pitia majina ya wafanyakazi wa hiyo kampuni pamoja na nafasi zao za kazi hapo.
  • Wapigie alafu muulizie afisa wa rasilimali watu au meneja wa ofisi alafu waulizi barua yako ya kazi itumwe kwa nani

3. Ufunguzi wa barua lazima iwe ya nguvu

Usipoteze muda wa mwajiri kwa kuanza na ‘Jina langu ni ______ na hii barua ni kuomba kazi ya __________ iliyotangazwa ZoomTanzania.

Badala yake, anza na sentensi ya nguvu. Kwa mfano:

“Kwa kuwa nimefanya kazi kwenye sekta ya Masoko, sekta ambayo ina mchakmchaka sana, kwa zaidi ya miaka 3 kwenye kampuni ya _________, nina uhakika wa kwamba mi ndio nitawafaa kujaza nafasi hii”

4. Kuwa na malengo

Badala ya kuongelea kazi zote ulizofanya maishani mwako, bora uongelee yale ambayo yatakusaidia kufanya kazi hii unayo omba.

Hii itasaidia kuweka picha kamilifu kwa mwajiri juu yako wewe, badala ya kuwajaza na maneno mengi yatakayoishia kuwachanganya.

5. Barua ni ya mwajiri, sio wewe

Hakikisha unaonyesha kwa uwazi kabisa namna gani utawasaidia wao na sio namna gani watakusaidia wewe.

Kwa mfano, badala ya kuandika ‘Kufanya kazi hapo _____ itaniwezesha kujiongezea ujuzi’ bora uandike ‘kama nitapewa nafasi ya kujiunga na kampuni yenu, nitatumia ujuzi wangu wa ______ kuchangia kwenye ukuaji wa kampuni hiyo’

6. Toa maelezo

Onyesha kwa kutumia mifano sifa zako.

Kwa mfano, badala ya kusema, ‘Mimi ninauwezo wa kuongoza’ toa mfano maalum ya uwezo huo kwa kusema, ‘Kwenye nafasi yangu ya _____ kwenye kampuni ya______ niliongoza idara iliyokuwa na watu wa 3 kwenye kazi ya _______ na ______’

7. Sisitiza uwezo wako

Mara nyingi tunajikuta tukikosa sifa chache zinazohitajika kwenye kazi tunaloomba, ila bado tunaamini kwamba tukipewa nafasi tutafanya vizuri.

Kwa hiyo, badala yakuonyesha kwamba umekosa ujuzi Fulani, onyesha uwezo na hamu ya kujifunza pamoja na jinsi gani utakavyokuwa jembe kwa kampuni.

8. Staili moja haiwafai wote

Usitumie barua moja kwa waajiri mbali mbali kwa kubadilisha jina ya kampuni tu. Maadili na changamoto kati ya makampuni zinatofautiana, hata kama ziko ndani ya sekta moja.

9. Fanya masahihisho

Muombe ndugu, jamaa au rafiki apitie barua yako na rekebisha makosa yote atakayokuta.

10. Hakikisha umeiandika kwa ufupi na uwazi

Barua yako ya kuomba kazi isizidi aya 4 na isiwe ndefu zaidi ya ukurasa mmoja.

Kumbuka, ingawa kuna vitu vingi amabavyo hatuwezi kudhibiti katika mchakato wa kuomba kazi, tunaweza kudhibiti ubora wa ombi letu la kazi.

Barua ya kuomba kazi iliyoandikwa kwa umakini na yenye malengo itakuongezea nafasi ya kuitwa kwenye interview. Hivyo, usilete mzaha!

Ila, kabla ya kuanza kuandika barua ya kuomba kazi:

Tafuta kazi unayotaka

Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment