JINSI YA KUFANYA WAFANYA KAZI WAKO WAZIDI KUKUONGEZEA FAIDA


0 Comments
2426

Tukija kwenye swala la furaha ya wafanyakazi, msemo wa kwamba ‘pesa hainunui furaha’ ni sahihi.  Zaidi ya hapo, pesa haiwahamasishi wafanyakazi kufanya kazi zaidi au kuongeza uaminifu wa mwajiri wao, kwao.

Unaweza ukafikiri kwamba mafanyakazi tija anapata motisha kwa pesa. Ukweli ni kwamba, mwajiri akimjali na kuwekeza kwenye msaada na furaha kazini – uzalishaji huongezeka.

Kwa kweli, utafiti kuhusu mambo yanayochangia wafanyakazi kubaki kwenye shirika za umma kwa muda mrefu Tanzania iligundua kwamba:

“Uhakika wa kazi, mafunzo, mishaara, mazingira ya kufanya kazi, uwezo wa kuchangia maamuzi, upatikanaji wa posho, uhusiano na wafanyakazi wenzio, pensheni na nafasi za kupandishwa cheo’ ndio zinahamasisha wafanyakazi kubaki kwenye shirika na kufanya kazi kwa bidii.

Hii ni taarifa muhimu kwa biashara zote, hasa kwa biashara za kitanzania, kwa kuwa wafanyakazi wanahamasishwa kwa hatua kali na kwa vitisho.

Sasa, ni jinsi gani unaweza kujenga mazingira ya kazini yaliyo na furaha kuwafanya wafanyakazi wapende kubaki daima, na pia, waweze kuongeza mapato yao? Zifuatayo ni njia 10 za kuanzia:

1. Usigombeze. Toa ushauri

Kila mtu anakosea na wafanyakazi wako watakosea pia. Ila, kwa kukosea wanaweza wakajifunza na wakawa wafanyakazi bora zaidi. Itakuwa vibaya zaidi wakiogopa kukosea tena na hivyo, kuacha kujaribu vitu vipya. Yote haya yanategemea namna gani utakavyo waonyesha wamekosea. Tunabidi tuwehuru kutoa maoni yetu bila kuogopa kwamba tutadharauliwa au tutagombezwa.

Inabidi waajiri wajue jinsi ya kumkosoa mfanyakazi kwa njia ambayo itamsaidia mfanyakazi kusuluhisha changamoto zake badala kumfanya aogope kukosea au ajisikie kwamba hana mtu wakuongea naye kuhusu changamoto zake.

2. Tambua juhudi za wafanyakazi

Wafanyakazi wanataka kujisikia kwamba juhudi zao zinathamaniwa na kutambuliwa na mabosi wao.

Kuwapongeza wafanyakazi waliofanikiwa kufikisha malengo yao ya mwaka na kufanya vizuri, ni kawaida kwa kampuni nyingi. Ila, kampuni chache sana zinawazawadia wafanyakazi hao. Makampuni chache zaidi ya hapo zinatambua wale ambayo hawajafanya vizuri kwa hali ya juu sana ila wameonyesha kuongezeka kwa kiwango chao kulinganisha na miezi kadhhaa yaliyopita.

Kwa hiyo, kuwa na ‘Mfanyakazi bora wa mwezi’ inaweza ikahamasisha wafanyakazi kuongeza bidii. Ila, ni vizuri zaidi kuwatambua na kuwapongeza wafanyakazi wote kwa michango ya mbalimbali na kuwakosoa kwa njia ya kuwasaidia ili waweze kujiboresha.

3. Ajiri wafanyakazi bora

Hili halina mjadala. Watu wanaoshindwa kufanya kazi zao vizuri watapata shida, watakosa furaha na hawata kuwa na mchango wa maana kwenye kampuni.

Jua namna ya kuajiri wafanyakazi bora, hapa

4. Lipa vizuri

Usiwapunje wafanyakazi wako. Toa nyongeza kulingana na jinsi gani mfanyakazi anafanikiwa na kazi zake, au wakati kampuni ikapata faida kubwa sana. Inabidi wafanyakazi wajisikie kwamba wanalipwa kulingana na kazi wanazozifanya na pia, kwamba wao nao wanafaidika pale kampuni inapofanikiwa zaidi.

5. Ofa faida nzuri nje ya mshaara

Hii inaweza ikawa bima ya afya, hela ya usafiri, gym n.k. Ila, kwa mwajiri anayetaka kuboresha uzalishaji wa wafanyakazi, michezo au chochote kinacho hamasisha wafanyakazi kukusanyika pamoja nje ya kazini inaweza ikasaidia.

6. Sehemu za kupumzika ni muhimu

Umuhimu wa kuweka chumba/vyumba ambapo wafanyakazi wanaweza kupeana mawazo inasaidia pia.

Vyumba hivyo vikiwa na fenicha nzuri, vitafunio na vinywaji zinaweza kusaidia wafanyakazi kwa kiasi kikubwa. Inasaidia kuweka mazingira ya kuongea kwa uwazi kuhusu kazi za ofisini. Mwisho wa siku, vichwa viwili ni nzuri zaidi ya moja kwenye maswala ya kuendeleza kampuni.

Pia, wafanyakazi wanatumia karibia muda wao wote wa wiki, kazini. Ofisi inakuwa kama nyumba yao kwa hiyo, haitakuwa mbaya wakiwa na sehemu nzuri ya kupumzika.

7. Onyesha kwamba kuna njia ya kujiendeleza kikazi

Wafanyakazi wakiacha kazi ni gharama kubwa kwa kampuni. Mfanyakazi akiondoka, inabidi mtu mwingine atafutwekujaza nafasi hiyo. Pia, inawezekana kwamba huyo mfanyakazi mpya anahitaji mafunzo. Yote haya yanatumia muda ambayo ingetumika kuongeza mapato kwenye kampuni.

8. Wafanyakazi wajisikie kwamba hawapo kazini kupokea mshaara tu

Kili mtu anataka kuchangia kitu hapa duniani.

Anthony Smith, Mkurugenzi Mtendaji na muanzilishi wa Insightly, anakubaliana na hii na kuliko yote mengine.

Kuwajulisha wanfanyakazi kuhusu maendeleo ya kampuni pamoja na mwelekeo wake itasaidi kuwapa furhaha wafanyakazi, hasa kwa kuwa watajiendeleza kadri kampuni inavyojiendeleza.

Kwa kufanya hivi, unaongeza uaminifu kati ya kampuni na wafanyakazi wako kwa kuwa watajisikia kwamba nao wanahusika kwenye kujenga na kuendeleza biashara hiyo kwa kuwa wao weneye wanajijenga na kujiendeleza kikazi.

9. Waombe wafanyakazi watoe maoni yao

Kwa kufanya hivi utapata maoni ya kuboresha kampuni yako na pia itawaonyesha wafanyakazi wako kwamba unajali maoni yao, hivyo kuwafanya waendelee kutoa maoni yao na kujisikia kwambamchango wao unathaminiwa.

10. Kufanya kazi na kupumzika ni muhimu

Hatumaanishi kwamba kila siku baada ya kumaliza kazi kunabidi kuwe na sherehe. Ila, sherehe mara moja ni vizuri. Kwa mfano, sherehe za:

  • Kila baada ya miezi kadhaa
  • Mitoko ya wote mara moja moja
  • Kujipongeza baada ya kufanikiwa na kazi kubwa iliyowahusisha wengi au iliyobadilisha kampuni kwa kiasi kikubwa

Kwa kuwapongeza na kuwazawadia wafanyakazi wako wakiwa wanastahili pongezo hizo, unawahamisha kufanya kazi kwa umakini wakati wakifurahia kazi na wakiwa na furaha kwa ujumla.

Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment