FAHAMU TAKWIMU YA UGONJWA WA COVID 19 (CORONA)

Silent COVID-19 Cases May Stymie Screening Efforts

APRILI 30, 2020
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha #COVID19 imeathiri takriban watu milioni 3.3 huku zaidi ya Wagonjwa 229,000 wakifariki dunia na wengine zaidi ya 923,000 wakipona

Marekani ndilo Taifa lililoathirika zaidi Ulimwenguni likiwa na jumla ya visa 1,159,028, vifo 62,631 huku wagonjwa waliopona wakiwa ni zaidi ya 91,447

Jumla ya visa hivyo inajumuisha katika Majimbo yote 50, na maeneo yote yaliyochini ya nchi hiyo pamoja na Wagonjwa waliorudi nchini baada ya kugundulika katika nchi nyingine, walio Magerezani na Jeshini

Jana, Aprili 29, 2020 Marekani imerekodi visa vipya 27,327 na vifo 2,611 ndani ya saa 24. Hata hivyo, namba hii inaweza kuongezeka sana kwa siku zijazo kutokana na kwamba nchi hiyo inaanza kuhesabu vifo vinavyodhaniwani vya #COVID19

Vifo vinavyodhaniwa ni vya #COVID19 ni vilivinavyotokea ambapo watu waliofariki wanahusishwa na #COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara
-
Idadi hiyo ya vifo inayoelezwa kupita idadi ya vifo vya Wanajeshi wa Marekani walikufa katika vita ya Vietnam (47,434), imepita makadirio ya vifo yaliyowekwa ambapo ikadiriwa vifo 60,000 vingevika Agosti 2020

APRILI 27, 2020
#CORONAVIRUS-UPDATES: Zaidi ya Wagonjwa 55,000 wamefariki nchini Marekani, ikiwa ni zaidi ya robo ya vifo vyote vilivyotokea Duniani

Huko Uingereza, Waziri Mkuu Boris Johnson anatarajiwa kurudi kazini leo baada ya kupona #COVID19. Aliruhusiwa kutoka hospitali Jumatatu ya Pasaka, Aprili 13, 2020

Aidha, nchini Uswizi baadhi ya Biashara zitaruhusiwa kufunguliwa leo, huu Italia ikipanga kulegeza baadhi ya masharti ya kupambana na CoronaVirus kuanzia Mei 4, 2020

Maduka ya maua, maduka ya vipodozi, na saluni, pamoja na hospitali zilizokuwa zimefungwa zitaruhusiwa kufunguliwa nchini Uswizi kuanzia leo huku watu wakitakiwa kufuata kanuni za usafi na umbali baina ya watu

APRILI 26, 2020
CORONAVIRUS: WATU ZAIDI YA 203,000 WAFARIKI DUNIA


Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), watu 203,921 duniani wamepoteza maisha kutokana na janga la COVID-19

Vilevile, takriban watu 2,955,469 ulimwenguni wana maambukizi ya Virusi vya COVID-19. Aidha, Wagonjwa 814,993 wamepona hadi kufikia sasa

Mataifa yaliyoathirika zaidi duniani ni Marekani, Uhispania, Italia, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza

Kwa upande wa Afrika, nchi zenye idadi kubwa ya waathirika mpaka sasa ni Afrika Kusini, Misri, Algeria, Cameroon na Ghana

NB: Takwimu zote ni hadi kufikia saa 2:50 asubuhi leo

UJERUMANI: IDADI YA MAAMBUKIZI YAFIKIA 154,175

Kwa mujibu wa Taasisi ya Robert Koch (RKI), Ujerumani imerekodi maambukizi mapya 1,737 na jumla ya waathirika nchini humo imefikia 154,175

Aidha, vifo vipatavyo 140 vimerekodiwa na jumla ya waliofariki dunia kutokana na Corona Virus ni 5,640. Ujerumani imepongezwa kwa namna ilivyokabiliana na maambukizi ya COVID-19, hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaopona ni kubwa kuliko ile ya wanaoambukizwa

Nchi hiyo ilianza kulegeza masharti Aprili 20 mwaka huu, japokuwa wataalamu wameonya kuwa maambukizi yanaweza kuongezeka kama watu hawatachukua tahadhari

APRILI 25, 2020
UINGEREZA: VIFO ZAIDI YA 20,000 VYAREKODIWA HOSPITALI


Vifo vipya 813 vilivyotokea Hospitali vimetangazwa na idadi ya Wagonjwa wa COVID19 waliofariki dunia katika Hospitali mbalimbali imefikia 20,319

Takwimu za vifo za Serikali hazihusishi vifo vilivyotokea nyumbani, nyumba za uangalizi au sehemu nyingine kwenye jamii.

Takwimu hizo hukusanywa tofauti na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kulingana na Hati za vifo

Uingereza imerekodi maambukizi 148,377 hadi kufikia leo

APRILI 24, 2020
UHISPANIA: VIFO VICHACHE ZAIDI VYAREKODIWA NDANI YA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA

Wizara ya Afya imetangaza vifo 367 ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni ndogo zaidi kutokea kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja. Uhispania imerekodi maambukizi 219,764 na vifo 22,524 hadi kufikia sasa

Waziri ya Afya, Salvador Illa amesema nchi hiyo ambayo imeongeza muda wa hali ya dharura mpaka Mei 09 mwaka huu itaendelea kuchukua tahadhari za kujikinga licha ya kuwepo na ongezeko dogo la maambukizi mapya ya Corona Virus

Aidha, kutokana na mwenendo wa mlipuko wa COVID-19 nchini humo, kuanzia Jumapili hii, watoto wataruhusiwa kutoka nje kwa muda wa saa 1 wakiwa chini ya uangalizi wa mzazi

BANGLADESH: MADAKTARI ZAIDI YA 200 WAAMBUKIZWA COVID19

Takriban madaktari 251 nchini Bangladesh wamepata maambukizi ya Corona Virus. Taasisi ya Madaktari (BDF) imelalamikia ukosefu wa vifaa kinga (PPE) kuwa chanzo cha Madaktari kupata maambukizi kutoka kwa wagonjwa

Kufuatia ongezeko la waathirika wa Corona nchini humo, Serikali imekuwa na changamoto ya kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi ya Virusi hivyo

Bangladesh, kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa kinga kwa ajili ya watoa huduma za afya. Nchi hiyo imerekodi maambukizi 4,186 na vifo 127 hadi sasa huku waliopona wakiwa 108

APRILI 23, 2020
MSALABA MWEKUNDU WASHAURI KUWEPO MIKAKATI YA KUSHUGHULIKIA MIILI YA WANAOFARIKI DUNIA

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imetoa wito kwa Serikali duniani kote kujiandaa na kuweka mikakati kwa ajili ya idadi kubwa ya watu wanaofariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID19

Imesema idadi kubwa ya vifo vinaweza kuzidi uwezo wa Mamlaka kushughulikia miili kwa ufasaha. Kamati hiyo imeeleza kuwa kukosa mikakati kunaweza kupelekea watu kuzikwa kwa pamoja, bila kuwa na rekodi ya nani amezikwa wapi

Pia imesema kuweka mipango haimaanishi watu wengi watafariki lakini ni muhimu iwepo ili kusaidia kupunguza majonzi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao

Vilevile, imeshauri Mamlaka kuwapa kipaumbele wanaoshughulika na miili hiyo kwa kuhakikisha wana vifaa kinga muhimu ili kulinda afya zao

APRILI 21, 2020
WHO YAONYA MATAIFA KUHARAKISHA KULEGEZA MASHARTI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuondoa masharti ya wananchi kutotoka nje ili kudhibiti COVID19 ni mchakato unaotakiwa kufanywa taratibu kwani kuharakisha kufanya hivyo kunaweza kuleta maambukizi upya

Mkurugenzi wa WHO Pasifiki ya Magharibi, Takeshi Kasai amesema masharti yameonekana kufanya kazi, na watu wanatakiwa kuwa tayari kwa mfumo huo mpya wa maisha wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la Coronavirus hadi pale chanjo an tiba itakapopatikana

Serikali zimetakiwa kuweka jitihada zaidi katika kudhibiti maambukizi, na WHO imeshauri masharti na tahadhari kulegezwa kwa namna ambayo italeta usawa kati ya kulinda afya za watu na kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea

UK: CHANJO YA CORONAVIRUS KUANZA KUJARIBIWA ALHAMISI

Wanasayansi kutoka Chuo cha Oxford ambapo chanjo ya ugonjwa wa COVID19 inatengenezwa wamesema kuna uwezekano chanjo hiyo ikafanikiwa kwa 80% lakini pia wamekiri inaweza kushindwa

Wamesema itaanza kujaribiwa rasmi kwa binadamu siku ya Alhamisi (Aprili 23, 2020) na majaribio hayo yatagharimu Paundi Milioni 20 (sawa na takribani TZS 56,952,036,140)

APRILI 20, 2020
UFARANSA: WAZIRI MKUU ASEMA HALI INABADILIKA, MAAMBUKIZI YAANZA KUPUNGUA


Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe amesema mwenendo wa ugonjwa wa COVID19 nchini humo unabadilika taratibu. Amesema dalili mojawapo kuwa mlipuko huo unaanza kupungua ni kushuka kwa idadi ya wagonjwa Hospitali

Ufaransa ni nchi ya nne kwa vifo vingi zaidi duniani kutokana na Corona Virus ikiwa imerekodi vifo 19,718 na maambukizi 152,894 hadi kufikia leo

Aidha, nchi hiyo ambayo imezuia wananchi wake kutoka nje kwa takriban wiki 5 sasa inatarajiwa kulegeza baadhi ya masharti kuanzia Mei 11 ambapo huenda biashara chache zikafunguliwa na watu kuruhusiwa kutoka huku wakiendelea kuchukua tahadhari

Hata hivyo, Philippe amesisitiza kuwa maisha hayatokuwa kama awali na watakaokutwa na COVID-19 watatakiwa kukaa nyumbani au katika hoteli zilizo chini ya uangalizi wa Serikali

UHISPANIA: WATU ZAIDI YA 200,000 WAATHIRIKA NA CORONAVIRUS

Wizara ya Afya ya Uhispania imesema nchi hiyo ina jumla ya maambukizi 200,210 ya COVID19 baada ya visa vipya 4,266 kurekodiwa leo. Kutokana na takwimu hizo, Uhispania inakuwa nchi ya pili kuathirika zaidi duniani nyuma ya Marekani

Mbali na ongezeko la wagonjwa, nchi hiyo pia imeripoti vifo vipya 399 na idadi ya waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa Coronavirus hadi kufikia sasa ni 20,852 huku waliopona wakiwa

Kwa upande wa Ulaya, Uhispania ina idadi kubwa zaidi ya waathirika wa Virusi vya Corona ikifuatiwa na Italia ambayo imerekodi maambukizi 181,228

APRILI 16, 2020
CALIFORNIA: WAUZAJI WA MAZIWA WAYATUPA KWA KUKOSA SOKO


Wauzaji wa maziwa katika Jimbo la California wanalazimika kutupa maziwa hayo baada ya soko kupungua kutokana na kufungwa kwa migahawa na shule

Mkurugenzi Mtendaji wa Western United Dairies, Anja Raudabaugh ambaye anawakilisha takriban Wafugaji 860 amesama baada ya agizo la kukaa ndani kutolewa, migahawa ilifungwa na asilimia 50 ya Wateja ilipotea kwa usiku mmoja

Amesema migahawa mikubwa kama TGI Friday’s na Applebee’s iliyokuwa ikichukua maziwa mengi na kuwa Wateja wakubwa kwa wafugaji, iliacha kununua maziwa tangu katikati ya mwezi Machi

Aidha, Wafugaji walipata pigo zaidi baada ya Shule kufungwa na vyakula vya mchana kutotolewa shuleni jambo linalowafanya kuwa na hifadhi kubwa ya maziwa kuliko mahitaji

APRILI 15, 2020
MAREKANI YAWEKA REKODI MPYA, WATU 2,228 WAFARIKI KWA SIKU 1


Marekani imerekodi idadi kubwa ya vifo 2,228 ndani ya saa 24 na kufikia vifo 28,368 hadi sasa kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha Reuters. Idadi kubwa ya awali ilikuwa Ijumaa ambapo vifo 2,069 vilirekodiwa

Nchi hiyo ambayo ni ya tatu kwa idadi kubwa ya watu duniani imerekodi Waathirika 606,194 hadi kufikia mapema leo idadi ambayo ni kubwa kwa mara tatu kwa nchi inayoifuata kwa Waathirika wa #COVID19

Ongezeko la vifo 2,228 halijumuishi makusudio ya Jiji la New York kujumuisha idadi ya vifo vinavyodhaniwa vimetokana na #CoronaVirus bila kupimwa

Mamlaka za New York zimeripoti vifo 3,778 vinavyodhaniwa ni kwasababu ya corona ambapo madaktari walijiridhisha ni kutokana na ugonjwa huo, na vifo 6,589 vilivyothibitishwa maabara. Ukijumlisha idadi hiyo ya vifo inafika zaidi ya 10,000

KENYA: IDADI YA WAATHIRIKA YAFIKIA 225. VIFO VYAFIKIA 10

Idadi ya waliopata maambukizi ya #COVID19 imeongezeka na kufikia 225 baada ya wagonjwa wapya 9 kuthibitika na virusi hivyo kufuatia kupimwa kwa sampuli 803 ndani ya saa 24

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wote wapya ni raia wa Kenya na hawana rekodi ya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa hivi karibuni. Ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa

Ameeleza kuwa kati ya wagonjwa hao wapya, watano wanatokea Nairobi na wanne wanatokea Mombasa na umri wao ni katika ya miaka 9 na miaka 69

Aidha, watu 12 wamepona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitalini; Idadi ya waliopona imefikia 53. Mtu mmoja amefariki kwa ugonjwa huo

Waziri amebainisha kuwa jumla ya watu 2,336 waliokutana na waathirika wamekuwa wakifuatiliwa, huku 1,911 wakiachiwa na wengine 455 wakiwa bado wanafuatiliwa

APRILI 14, 2020
KUNDI LA WACHUNGAJI LAMSHTAKI GAVANA WA CALIFORNIA KWA KUZUIA MIKUSANYIKO YA KIDINI


Kundi la Wachungaji kutoka Kusini mwa Jimbo la California limemshtaki Gavana Gavin Newsom na baadhi ya Watendaji kwa kuzuia Waumini kwenda Kanisani kutokana na #CoronaVirus

Mashtaka hayo yamefunguliwa jana katika Mahakama ya huko California na Kampuni ya Kisheria ya Dhillon, kwa niaba ya Walalamikaji wanne na watatu kati yao ni Wachungaji

Walalamikaji ni Dean Moffatt, Mchungaji katika Kanisa la Indio anayedaiwa kupigwa faini ya $1,000 kwa kuongoza Ibaya ya Jumapili ya Matawi; Brenda Wood, Mchngaji wa Kanisa la Riverside; Patrick Scales, Mchungaji wa Kanisa la Fontana na Wendy Gish Muumini wa kanisa la Fontana

Walalamikaji hao pia wanamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Jimbo, Xavier Becerra na baadhi ya Watendaji wa Kaunti za Riverside na San Bernardino wakiwemo Polisi na Wafanyakazi wa sekta ya Afya

Machi 19, Newsom alitoa agizo la kwanza la kuwataka Wakazi takriban milioni 40 wa California kukaa nyumbani ili kupunguza kusambaa kwa virusi hiyo

APRILI 13, 2020
ASILIMIA 18 YA POLISI WA NEW YORK WAHOFIWA KUUNGUA #COVID19


Takriban Polisi 6,522 wa Idara ya Polisi ya New York hawakuweza kufika kazini siku ya jana kwa mujibu wa ripoti ya kila siku ya #CoronaVirus ya Idara hiyo

Ripoti hiyo imeeleza kuwa hadi sasa Polisi 2,344 na Wafanyakazi wasio Polisi 489 wa Idara hiyo ndio wamethibitika kuwa na ugonjwa wa #COVID19

Ongezeko la Wagonjwa 5,695 kwa siku ya jana kumefanya New York kuwa na zaidi ya Waathirika 104,000 na takriban vifo 6,182 vilivyorekodiwa

Kwa ujumla Marekani ndio nchi iliyoathirika zaidi duniani na virusi hivi ikiwa na jumla ya Waathirika 560,433 huku ikiwa imesharipoti vifo 22,115

APRILI 12, 2020
MAREKANI YAIZIDI ITALIA KWA VIFO


Marekani imeipita Italia kwa vifo ikiwa imerekodi vifo 20,602 na ikiwa na Waathirika takriban 529,740 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins

Waathirika hao wapo katika Majimbo yote 50 ikiwemo ‘District of Columbia’ hadi sasa Jimbo pekee ambalo halijatangaza kifo cha mgonjwa wa #COVID19 ni Wyoming pekee

Takriban nusu ya vifo hivyo vimetokea New York ambapo Gavana wa sehemu hiyo, Andrew Cuomo amesema Jana kuwa Ijumaa kulitokea vifo 783 na kufanya Jimbo hilo kuwa na vifo 8,627

Aidha, kwa mujibu wa takwimu, Marekani ilikuwa na vifo 58 wiki nne zilizopita, na katika wiki 3 zilizopita ilikuwa na vifo 323. Katika wiki mbili zilizopita vifo vilifika 2,043 na wiki moja iliyopita kulikuwa na vifo 8,488

Jana, Aprili 10, 2020 Italia ilitangaza jumla ya vifo 619 vipya vinavyohusiana na #COVID_19 na kufanya Taifa hilo la Ulaya kuwa na jumla ya vifo 19,468

KENYA: MAAFISA 6 WA AFYA WAPATA MAAMBUKIZI YA #COVID19 WAKIWA KAZINI

Kwa mujibu wa Umoja wa Maafisa Kliniki wa Kenya (Kenya Union of Clinical Officers), maafisa afya wapatao 6 wamepata maambukizi ya #COVID19 wakiwa kazini

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini humo umebaini 68% ya wafanyakazi wa sekta ya afya ya jamii hawana mafunzo maalum ya kukabiliana na wagonjwa wa #CoronaVirus

Katibu wa Umoja huo amesema upungufu wa barakoa na glovu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vilivyochangia maafisa hao sita kupata maambukizi

APRILI 11, 2020
ITALIA: TAKRIBAN MAPADRI 100 WAFARIKI DUNIA KWA CORONA VIRUS


Mapadri hao wamefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya COVID-19. Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya Viongozi hao wa Dini walikuwa wastaafu

Mapadri wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutoa huduma za kiroho kwa wazee na Waumini walioathirika zaidi na Ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali

Nchi ya Italia ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa Coronavirus ikiwa na maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia jioni ya leo

MAREKANI: CORONA VIRUS YAGHARIMU MAISHA YA WATU 2000 NDANI YA SIKU MOJA

Watu 2,018 wamefariki dunia kutokana COVID-19 ndani ya siku moja, idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi kurekodiwa duniani

Huenda nchi ya Marekani yenye waathirika 503,177 na vifo 18,761 hadi sasa ikaipiku Italia ambayo imerekodi vifo 18,849 kufikia leo kwa kuwa na vifo vingi zaidi

Licha ya ongezeko hilo la vifo, Wataalamu wa Kikosi Kazi cha COVID-19 kutoka Ikulu wanasisitiza kuwa makali ya mlipuko huo yameanza kupungua

Rais Donald Trump naye amesema anatarajia kuona vifo vichache zaidi vikirekodiwa tofauti na makadirio yaliyotolewa awali

KOREA KUSINI: WAGONJWA 91 WALIOPONA COVID-19 WAPATA MAAMBUKIZI

Mamlaka za Korea Kusini zimeripoti kuwa takriban watu 91 waliopona Corona Virus wamepata maambukizi kwa mara ya pili

Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo, Jeong Eun-kyeong amesema kuna uwezekano mkubwa virusi hivyo vilikuwa vimelala (dormant) na sio kwamba watu hao wameambukizwa upya

Aidha, Wataalamu wanasema huenda vipimo walivyofanyiwa watu hao vilionesha majibu ya uongo au baadhi ya virusi vilibaki mwilini ila havikuwa na madhara

Hata hivyo, Wataalamu wa Afya wa Korea Kusini bado hawajafahamu kinachosababisha hali hiyo na undani wa jambo hilo unaendelea kuchunguzwa

Hali ya wagonjwa wa Corona kupata maambukizi baada ya kupona ni suala ambalo linahofiwa kimataifa kwakuwa nchi nyingi zinatamani walioathirika watakuwa na kinga ya mwili ya kutosha itakayowazuia kuambukizwa tena

ITALIA KUBAKI KARANTINI HADI MWEZI MEI

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte ametangaza kuwa muda wa wananchi kutotoka nje umeongezwa hadi Mei 3 ili kudhibiti maambukizi mapya ya COVID-19

Italia ambayo imerekodi maambukizi 147,577 na vifo 18,849 hadi kufikia leo tayari imekuwa chini ya amri hiyo kwa mwezi mmoja ma wananchi wametakiwa kubaki nyumbani

Akitangaza uamuzi huo, Conte amesema wakiacha kuchukua tahadhari zaidi, watahatarisha maendeleo waliyopata mpaka sasa na kusababisha vifo zaidi

APRILI 10, 2020
UINGEREZA: BORIS JOHNSON ATOLEWA ICU


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodini huku bado akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalum

Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imeeleza kuwa Johnson ambaye alilazwa baada ya hali yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri hivi sasa.

Wanasayansi wametahadharisha kuwa Uingereza inaingia katika hatua mbaya zaidi ya mlipuko wa #Covid19 na wanatarajia vifo vingi zaidi kurekodiwa kuelekea sikukuu ya Pasaka

Jumla ya maambukizi 65,077 na vifo 7,978 vimerekodiwa hadi kufikia leo

APRILI 09, 2020
UHISPANIA KULEGEZA MASHARTI, WAZIRI MKUU ASEMA KIPINDI KIGUMU KINAPITA


Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez amesema nchi hiyo inatarajia kulegeza masharti ya karantini yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi na Virusi vya Corona

Sanchez ambaye pia ameombe Bunge kupitisha ombi lake la kuongeza muda wa hali ya tahadhari mpaka Aprili 26 amesema kutokana na athari zilizosababishwa na janga la Covid-19, mchakato wa maisha kurejea kama zamani utachukua wa taratibu

Uhispania ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi na janga la Corona Virus baada ya Marekani. Maambukizi 152,446 na vifo 15,238 vimerekodiwa huku wagonjwa 52,165 wakipona hadi kufikia leo

Mbali na Uhispania, mataifa mengine ya Ulaya nayo yanakifikiria kulegeza masharti mapema iwezekanavyo kutokana na wasiwasi wa uchumi kuathirika kwasababu ya kuwekwa kwa amri ya karantini

APRILI 08, 2020
UINGEREZA: WAZIRI MKUU BORIS JOHNSON APATA NAFUU

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (55) aliyewekwa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London baada ya afya yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri baada ya kupatiwa Oxygen

Johnson aliyegundulika kuwa na maambukizi ya #Covid19 wiki mbili zilizopita alifikishwa Hospitali Jumapili. Alihamishiwa ICU baada ya hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imesema anaendelea vizuri na hajawekewa mashine za kupumulia

Kwa muda ambao Johnson amelazwa Waziri wa Mambo ya Nje, Dominic Raad ataongoza harakati za kudhibiti maambukizi ya Corona na amepewa baadhi ya mamlaka ya Waziri huyo. Hata hivyo, maamuzi yote makubwa ikiwemo kusitisha karantini yatapitishwa na Baraza

Endapo Raad atashindwa kazi hiyo, Waziri wa Fedha Rishi Sunak (39) atapewa mamlaka

MAREKANI: WATU 1,736 WAFARIKI DUNIA NDANI YA SAA 24

Marekani imeripoti vifo 1,736 vilivyotokea Jumanne, idadi kubwa zaidi kurekodiwa ndani ya siku moja, ambapo asilimia kubwa ya vifo hivyo vimetokea Jijini New York

Jumla ya waliofariki kutokana na Virusi vya Corona imefikia 12,854. Maambukizi yaliyorekodiwa nchini humo mpaka sasa ni 400,412, idadi ambayo ni kubwa zaidi duniani

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha kutoa fedha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) huku akilishutumu Shirika hilo kwa kuipendelea China na kushindwa kudhibiti mlipuko huo ambao umegharimu maisha ya watu 82,080 duniani kote

Trump amesema WHO imefanya makosa na ilitakiwa kutangaza tahadhari mapema zaidi huku akidai kuwa walitakiwa kufahamu athari za mlipuko wa #Covid19 mapema zaidi, hivyo Marekani itafanya tathmini juu ya fedha ambazo inatoa kwa Shirika hilo

APRILI 07, 2020
MADAKTARI 94 NA WAUGUZI 26 WAFARIKI DUNIA


Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 07, 2020 na Umoja wa Madaktari nchini humo huku Shirikisho la Wauguzi likisema licha ya Wauguzi 26 kufariki wengine 6,549 wanaugua #COVID19

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya nchini humo, hadi kufikia jana Aprili 06, 2020 jumla ya Wafanyakazi 12,681 wa sekta ya Afya walikuwa wanaugua ugonjwa huo

Inaelezwa kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona umesababisha idadi ya wafanyakazi wanaougua ugonjwa huo kuongezeka

Mojawapo ya miundombinu bora ya afya barani Ulaya ipo Kaskazini mwa Italia lakini imeshidhwa kukidhi kuhimili wingi wa wagonjwa wa #COVID_19 wanaogundulika nchini humo

Italia imeripoti jumla ya waathirika 132,547, idadi ya vifo 16,523 na waliopona hadi sasa ni 22,837

MAREKANI: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA

Idadi ya vifo ambayo imerekodiwa Marekani hadi asubuhi ya leo ni 10,876. Nchi hiyo inakuwa ya tatu kwa vifo vingi zaidi duniani baada ya Uhispania (13,341) na Italia (16,523)

Wataalamu wa Afya kutoka Ikulu ya Marekani wametabiri kuwa watu 100,000 hadi 240,000 wanaweza kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID-19 hata kama maagizo ya kukaa nyumbani yakifuatwa

Marekani imesema hali inaweza kuwa mbaya wiki hii, ambapo maambukizi na vifo vingi vitarekodiwa. Miji ya New York, New Jersey, Connecticut na Detroit inatajwa kuwa katika hatari zaidi

Hadi sasa, takriban asilimia 90 ya Wamarekani wanatekeleza agizo la kukaa nyumbani na kuepuka mikusanyiko huku majimbo nane yakiwa bado hayajatoa tamko hilo

NEW ZEALAND: WAZIRI WA AFYA ASHUSHWA CHEO BAADA YA KUIPELEKA FAMILIA BAHARINI WAKATI WA KARANTINI

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amemshusha cheo Waziri wa Afya David Clarke kwa kukiuka taratibu zilizowekwa kudhibiti maambukizi ya #Coronavirus nchini humo na kuipeleka familia yake baharini

Waziri Ardern amesema katika mazingira ya kawaida angemfukuza kabisa kazi Clarke kwasababu kitendo alichofanya sio sawa na alitarajia atakuwa mfano kwa wengine

Clarke ametolewa katika nafasi yake ya Waziri wa Afya na sasa atakuwa katika nafasi za chini za Baraza. Katika taarifa yake, amesema hakutumia busara na anaelewa kwanini watu wamekasirishwa

New Zealand yenye watu Milioni 5 ilitangaza karantini ya nchi nzima mwishoni mwa mwezi uliopita na kufunga mipaka yake, shule, migahawa pamoja na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu

Idadi ya maambukizi iliyoripotiwa nchini humo ni 1,160 na mpaka sasa kifo kimoja kimerekodiwa

APRILI 06, 2020
UHISPANIA: IDADI YA VIFO YAPUNGUA KWA SIKU NNE MFULULIZO

Idadi ya vifo vilivyorekodiwa kutokana na maambukizi ya #Covid19 imeendelea kupungua kwa siku ya nne sasa, hali ambayo inaleta matumaini kuwa Uhispania imemaliza kipindi kigumu

Uhispania yenye jumla ya waathirika 135,032 ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi Ulaya. Vifo 637 vimeripotiwa leo na idadi ya jumla waliofariki dunia hadi sasa ni 13,055

Mbali na Uhispania, vifo nchini Italia, Ufaransa na Ujerumani pia vimeendelea kupungua. Hii inaashiria kuwa mkakati wa watu kuwekwa karantini na kuzuia mikusanyiko umesaidia kupunguza maambukizi

Maambukizi 1,287,168 ya Virusi vya Corona yameripotiwa duniani. Watu 70,530 wamepoteza maisha kutokana na Virusi hivyo na waliopona hadi leo ni 271,887

APRILI 05, 2020
MAREKANI: WATU 1,344 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. HALI MBAYA ZAIDI YAHOFIWA


Marekani imetangaza idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na #COVID19 kwa siku moja huku Wataalam wakitahadharisha kuwa wiki mbili zijazo zitakuwa mtihani mkubwa katika kupambana na maambukizi nchini humo

Nchi hiyo imetangaza jumla ya vifo 1,344 vilivyorekodiwa kutokea jana Aprili 04, ikiwa ndio idadi kubwa ya vifo kutokea ndani ya saa 24 kwa Taifa moja tangu kulipuka kwa Ugonjwa huo

Idadi hiyo inapelekea Marekani kuwa na jumla ya vifo 8,496 huku kukiwa na jumla ya Waathirika 312,076, idadi kubwa ya Waathirika kuliko Taifa lolote

Mratibu wa Timu ya kukabiliana na CoronaVirus ya Ikulu ya Marekani, Dkt. Deborah Birx ametahadharisha kuwa siku chache zijazo Marekani itashuhudia mtihani wake mkubwa na zitakuwa siku muhimu sana katika mapambano hayo

Amesema “Hizi ni siku za kutokwenda dukani, kutokwenda duka la dawa, na fanya lolote uwezalo unalodhani litaiweka familia yako na marafiki zako salama na hii ni kila mtu kuhahikisha anakaa umbali wa Mita 2 kutoka kwa mwenzako na unanawa mikono”

Aidha, Rais Donald Trump ameaambia Wamarekani kujiaandaa na ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na #Corona katika kile alichokiita wiki mbili ngumu zijazo katika mapambano na mlipuko huo

UHISPANIA: WATU 674 WAFARIKI KWA SIKU 1. IDADI NDOGO KUTOKEA TANGU MAPEMA MACHI

Watu wengine 674 wamefariki kwa #COVID19 nchini humo kwa siku ya jana Aprili 04, ikiwa ni idadi ndogo zaidi kutokea ndani ya saa 24 tangu mwezi Machi 2020

Nchi hiyo kwa sasa ina jumla ya vifo 12,418 vilivyorekodiwa ikiwa ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya Italia iliyorekodi jumla ya vifo 15,362

Pamoja na kuwa ya pili kwa vifo, takwimu zinaonesha Taifa hilo linaelekea kumaliza kipindi kigumu zaidi cha mlipuko wa ugonjwa huo ambapo sasa idadi ya vifo na Waathirika wapya inayorekodiwa inapungua

Wizara ya Afya imesema leo kuna jumla ya Wagonjwa 80,261 wa #COVID19, ikiwa idadi hiyo imeongezeka kwa Wagonjwa 1,488 kutoka Jumamosi lakini pia ndio ongezeko dogo kwa siku tangu Machi 17

Ila pia Wizara hiyo imeripoti kuwa jumla ya Wagonjwa 38,080 wamepona ugonjwa huo ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 4,000 kutoka idadi iliyoripotiwa jana Aprili 04, 2020

APRILI 03, 2020
#CORONAVIRUS-UPDATE:
 Idadi ya Watu walioathirika na maambukizi ya virusi vya #COVID19 imezidi milioni moja Ulimwenguni kwa mujibu wa Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins

Nchi tano zenye Waathirika wengi waliorekodiwa ni Marekani (245,184), Italia (115,242), Uhispania (112,065), Ujerumani (84,794) na China (81,620)

Lakini pia nchi tano zenye idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa ni Italia (13,915), Uhispania (10,348), Marekani (6,088), Ufaransa (5,387) na China (3,322)

UHISPANIA: WATU 932 WAFARIKI NDANI YA SAA 24

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 03, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,935

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 932 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Jana, Wizara hiyo ilitangaza vifo 950 vilivyotokea ndani ya saa 24

Aidha, data za Wizara hiyo zinaonesha kuwa kuna Wagonjwa 76,262 kwa sasa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa 2,770 kutokea idadi ya jana lakini pia ni ongezeko dogo tangu Machi 20

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,915. Inashika nafasi ya pili kwa Waathiriki ikiwa na Waathirika 117,710 nyuma ya Marekani (245,380)

APRILI 02, 2020
UHISPANIA: WATU 950 WAFARIKI NDANI YA SAA 24


Kwa mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini humo leo Aprili 02, 2020, jumla ya Watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID19 imefikia 10,003

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 950 vya Wagonjwa wa #Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Hii ni idadi kuwa ya vifo kwa siku moja kutokea nchini humo

Uhispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa Ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,155. Pia, ikiwa na maambukizi 110,238 inazifuata nchi za Marekani (215,344) na Italia (110,574) kwa maambukizi mengi

BALOZI WA UFILIPINO NCHINI LEBANON AFARIKI KWA #COVID19

Bernardita Catalla aliyekuwa Mwanadiplomasia kwa miaka 27, amefariki katika hospitali iliyopo Beirut baada ya kuugua ugonjwa wa #Covid_19

Miezi kadhaa nyuma, Balozi huyo aliongoza mpango wa kuwaondoa takriban Wafilipono 2,000 nchini Lebanon, wengi wakiwa ni Wanawake waliokuwa wakifanya kazi za ndani

Tangu Oktoba 2019, Lebanon imekuwa na migogoro ya Kisiasa na Kifedha na Wakimbizi wengi wa Kiafrika na bara la Asia wanaofanya kazi nchini humo wanalalamika kulipwa kidogo au kucheleweshewa mishahara

APRILI 01, 2020
AFRIKA: WATU 203 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19


Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa vya Umoja wa Afrika kimesema kuwa watu 203 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya #Covid19

Hadi sasa #CoronaVirus imeenea katika nchi 50 barani Afrika na jumla ya maambukizi 5,886

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maambukizi nchini Lesotho, Sudani Kusini, visiwa Sao Tome na Principe, Comoro na Malawi

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya maambukizi, ikiwa imefikia 1,353, huku watu saba wakiwa wamethibitishwa kufariki kwa #Covid19

KENYA: WAGONJWA WAPYA 22 WATHIBITISHWA. MAAMBUKIZI YAFIKIA 81

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 22 wamekutwa na #CoronaVirus leo ambapo idadi hii inafanya jumla ya maambukizi kufikia 81

Kati ya wagonjwa hao 22, 18 ni raia wa Kenya, 2 raia wa Pakistan na 2 ni raia wa Cameroon. Aidha 13 kati yao ni wanaume na 9 ni wanawake

Waziri amesema wagonjwa hao wapya wamepatikana baada ya Watu 300 kupimwa na kuwa kati ya hao 22, 21 walikuwa Karantini tayari

MACHI 30, 2020
ITALIA: WATU 756 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. IDADI YA VIFO ILIYOREKODIWA YAFIKIA 10,779


Idadi ya vifo kwa Italia ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi yoyote nyingine na vifo hivyo vinachukua theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 33,982

Licha ya kutokea kwa vifo 756 Jumapili, idadi ya vifo nchini humo imeonekana kupungua ambapo Jumamosi kulirekodiwa jumla ya vifo 889 na Ijumaa vifo 969 vilirekodiwa

Aidha, Idadi ya maambukizi kwa Jumapili yalifikia 97,689 kutoka 92,472 ikiwa ni kiwango kidogo cha maambukizi kuongezeka tangu Jumatano Machi 25, 2020

Kati ya wale walioambukizwa nchi nzima, 13,030 walikuwa wamepona kufikia Jumapili, ikilinganishwa na 12,384 waliokuwa wamepona Jumamosi. Watu 3,906 walikuwa ICU ikilinganishwa na 3,856 waliokuwepo siku iliyopita

MAREKANI: RAIS TRUMP AONGEZA MUDA WA WATU KUKAA NDANI

Rais Donald Trump amesema muda wa watu kujitenga kwa kukaa ndani na kutokusanyika umeongezwa hadi Aprili 30 baada ya Wataalamu kuonya kuwa vifo vinaweza kufika 100,000

Amesema, "Inakadiriwa kuwa vifo vingi vinaweza kutokea kwenye wiki mbili zijazo. Hivyo kwa wiki mbili hizo na katika kipindi hiki ni muhimu watu kufuata kanuni hizo"

Ameongeza, "Kama idadi ya vifo itabaki katika 100,000 au pungufu ya hapo (Marekani), wote tutakuwa tumefanya kazi kubwa. Hivyo ni bora kila moja kufuata Kanuni hizo ili janga hili liishe mapema."

Aidha, katika hatua nyingine Trump amesema Usalama wa Taifa walimzuia kwenda New York (Mji unaoongoza kwa maambukizi Marekani) kuhudhuria ufunguzi wa hospitali ya wagonjwa wa #COVID19

Hospitali hiyo ya muda katika Kituo cha Javits inatarajiwa kuwa na vitanda takriban 2,900 ii kukabiliana na wimbi la Wagonjwa wa #COVID_19 wanaoongezeka kwa kasi

UHISPANIA: WATU 812 WAFARIKI NDANI YA SAA 24. YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI

Mamlaka zimeripoti kuwa pamoja na vifo hivyo kumekuwa na jumla ya ongezeko la wagonjwa 3,515 ndani ya saa 24 na kufanya idadi ya Wagonjwa waliorekodiwa kufikia 61,075

Jumla ya Idadi ya vifo vilivyoripotiwa nchini humo imefikia 7,340 kutoka vifo 6,528 vilivyoripotiwa Jumapili. Ni nchi ya pili kwa vifo vingi baada ya ya Italia yenye vifo 10,779

Nchi hiyo imeripoti jumla ya maambukizi 85,195 kutoka 78,797 yaliyokuwepo Jumapili na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi mengi kuliko China yenye maambukizi 81,470

Aidha, wagonjwa 2,071 wamepona katika saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya watu waliopona kuwa 16,780. Katika muda huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 324 waliokuwa wakihitaji uangalizi maalumu

ITALIA: MADAKTARI 61 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA MAAMBUKIZI

Kwa mujibu wa Chama cha Madaktari nchini humo, Madaktari 61 wamefariki dunia huku Wafanyakazi wengine 8,358 wa sekta ya Afya wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo

Kati ya Madaktari hao 61, 40 walikuwa wakifanya kazi katika Mji wa Lombary ambao ndio chimbuko la virusi hivyo Italia na ndiko kwenye maambukizi mengi

Nchi hiyo ikiwa imerekodi jumla ya maambukizi 97,689 ina karibia kuwa nchi ya pili kuwa na maambukizi mengi yaliyozidi 100,000 baada ya Marekani yenye maambukizi 144,410

Aidha, nchi hiyo ina jumla ya vifo 10,779 vilivyorekodiwa na vikiwa vinachukua takriban theluthi moja ya jumla ya vifo vyote vya #Covid19 duniani ambavyo ni 35,339

MACHI 29, 2020
CORONAVIRUS MAREKANI: MJI WA NEW YORK KUTOWEKWA KARANTINI


Rais Donald Trump amesema Mji wa New York wenye maambukizi mengi Marekani (53,455) hautawekwa karantini na kuagiza Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) kutoa maelekezo kwa wasafiri

Uamuzi wake unakuja siku chache baada ya kutangaza kuwa anafikiria kuiweka Miji ya New York, New Jersey (maambukizi 11,124) na Connecticut (maambukizi 1,524) karantini ili kuzuia maambukizi ya #COVID_19

Awali, Gavana wa New York, Andrew Cuomo alipinga Mji huo kuwekwa karantini na kudai soko la hisa litaporomoka vibaya na itachukua miezi kama sio miaka kwa uchumi wa Marekani kurudi kama ulivyokuwa

Baada ya agizo hilo, CDC imewataka wananchi kutoka Miji hiyo mitatu kusitisha safari zote za ndani zisizo na umuhimu kwa muda wa siku 14. Agizo hilo halitawahusu watoa huduma za chakula, afya na fedha

ITALIA: WATU ZAIDI YA 10,000 WAFARIKI DUNIA KWA #CORONAVIRUS

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Italia imefikia 10,023 baada ya vifo 889 kuripotiwa Jumamosi

Mbali na vifo hivyo, maambukizi mapya 5,974 pia yameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita na nchi hiyo ina jumla ya maambukizi 92.472 mpaka sasa

Italia ina wagonjwa 70.065 na kati yao 66,209 wana hali nzuri huku wengine 3,856 wakiwa na hali mbaya. Wagonjwa waliopona #COVID_19 ni 12.384

Nchi hiyo itashusha bendera nusu mlingoti katika miji mbalimbali Machi 31 mwaka huu, ili kuwaenzi waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo

MACHI 27, 2020
CORONAVIRUS: MAREKANI YAIZIDI CHINA KWA IDADI YA MAAMBUKIZI


Marekani imeripoti jumla ya maambukizi 85,594 na kuwa nchi yenye maambukizi mengi zaidi ikiizidi China yenye maambukizi 81,340 na Italia yenye maambukizi 80,589

Hata hivyo italia bado inaongoza kwa vifo vilivyotokana na #Covid_19, ikiwa imetangaza vifo 8,215 ikifuatiwa na Uhispania yenye vifo 4,365 huku Marekani ikiwa na vifo 1,300 na China kuna vifo 3,292

Huko Chicago katika Gereza la Cook County lenye Wafungwa 5,400, Wafungwa 24 wamepatikana na mambukizi ya virusi vya #corona baada ya Wafungwa 89 kuonesha dalili kama za mafua na kupimwa

Aidha, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti ameonya kuwa kwa namna maambukizi yanavyoongezeka California yenye maambukizi 4,044 inaelekea kuwa New York huku New York yenye maambukizi 38,977 inaenda kuwa kama Italia

MACHI 26, 2020
CORONAVIRUS: MWANADIPLOMASIA WA UINGEREZA AFARIKI. MAREKANI YAIDHINISHA USD TRILIONI 2


Mwanadiplomasia wa Juu wa Uingereza, Steven Dick (37) aliyekuwepo nchini Hungary amefariki Jumanne Machi 24, baada ya kupata maambukizi ya #Covid_19

Hungary ina jumla ya maambukizi 261, Vifo 10 na waliopona 28 huku Uingereza ikiwa na jumla ya maambukizi 9,529, vifo 465 na waliopona 135

Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha Dola za Kimarekani Trilioni 2 kwa ajili ya kusaidia mifumo ya afya, wafanyakazi na biashara zilizoathiriwa na mlipuko wa #corona

Marekani ina jumla ya maambukizi 68,489, vifo 1,032 na waliopona ni 394. Nchi hiyo ina idadi ya Watu milioni 329 na Watu 418,810 wamepimwa hiyo inamaanisha mtu mmoja kati ya 785 ameathirika

Serikali ya Urusi imeiagiza Mamlaka ya Anga nchi humo kusitisha safari zote za Kimataifa za ndege zinazoingia na kutoka nchini humo kuanzia Kesho Machi 27

Thailand imetangaza maambuki maambukizi mapya 111 na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi 1,045 huku ukizuia wale wote wasio raia, Wanadiplomasia au wenye vibali vya kutofanya kazi nchini huko kutoingia


MACHI 25, 2020
CORONAVIRUS: UINGEREZA YAWATAKA WATU KUKAA NDANI. MIKUSANYIKO ZAIDI YA WAWILI MARUFUKU

Watu wanaweza kwenda kufanya mazoezi nje ya nyumba mara moja kwa siku, kusafiri kwenda na kurudi ofisini panapo ulazima, kwenda dukani kwa mahitaji muhimu na kwenda hospitali

Maduka yanayouza bidhaa zisizo za muhimu yametakiwa kufungwa na mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili katika maeneo ya wazi imezuiwa. Watu wa familia moja ndio wameruhusiwa kukaa pamoja ndani

Iwapo watu hawatafuata maagizo hayo, Polisi wana mamlaka ya kushinikiza yafuatwe ikijumuisha kutawanya mikusanyiko na kuwatoza faini watu hao

Waziri Mkuu Boris Johnson amesema nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali ya dharura na hivyo watu kukaa nyumbani ni suala la muhimu. Hali hiyo itaendelea kwa wiki tatu chini ya uangalizi

Kwa sasa Uingereza ina jumla ya maambukizi 8,077 na jumla ya vifo ni 422 huku kukiwa na Wagonjwa 135 waliopona


ITALIA YATANGAZA VIFO 743 NDANI YA SAA 24. WHO YAITAHADHARISHA MAREKANI

Hali imeendelea kuwa mbaya nchini Italia baada ya nchi hiyo kutangaza vifo vya watu 743 ndani saa 24 zilizopita na kufanya nchi hiyo kuwa na jumla ya 6,820 vya Wagonjwa wa #covid_19

Hata hivyo, siku mbaya zaidi kwa nchi hiyo ambayo imetangaza kuwa na Maambukizi 69,176 kwa Jumanne kutoka 63,919 kwa Jumatatu, ilikuwa ni Jumamosi ilipotangaza vifo 793

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeitahadharisha Marekani yenye Maambukizi mengi baada ya China na Italia kuwa inaweza kuwa kitovu kipya cha Maambukizi huku Trump akisisitiza kuwa watarudi kazini baada ya wiki 3

Hadi sasa Marekani ina jumla ya maambukizi 54,867 katika Majimbo yake yote 50 huku kukiwa na jumla ya vifo 782. China ina maambukizi 81,218 na vifo 3,281
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
3,572
2,000
MEI 25, 2020
UHISPANIA: WATALII KURUHUSIWA KUANZIA JULAI 1

Uhispania imewataka watalii kurejea nchi humo kuanzia Julai 1 mwaka huu baada ya masharti yaliyowekwa nchini humo ili kudhibiti COVID19 kuanza kulegezwa

Waziri wa Utalii, Reyes Maroto amesema ni sawa kupanga kwenda nchini humo kwa ajili ya likizo kuanzia Julai. Kufuatia mwenendo wa COVID19, inawezekana amri ya wageni kukaa karantini ya lazima kwa siku 14 ikatolewa

Uhispania ambayo ni nchi ya pili kutembelewa zaidi duniani hupata wageni takriban Milioni 80 kwa mwaka inajipanga kufungua sekta ya utalii

Mpaka sasa visa 282,852 vimerekodiwa nchini humo, waliopona ni 196,958 na vifo ni 28 752

MEI 22, 2020
UHISPANIA: MASHARTI MADRID, BARCELONA KULEGEZWA KUANZIA JUMATATU

Serikali imesema masharti yaliyowekwa kudhibiti COVID19 katika miji ya Madrid na Barcelona yataanza kulegezwa kuanzia Jumatatu ijayo baada ya maambukizi kupungua

Mapema mwezi huu, masharti yalilegezwa katika maeneo mengine ya nchi hiyo lakini Miji hiyo miwili iliendelea kufuata taratibu zote za wawili kwakuwa iliathirika zaidi na CoronaVirus

Migahawa na baa itaruhusiwa kutoa huduma kwa nusu idadi, makanisa nayo yatafunguliwa na wananchi wataruhusiwa kusafiri nje ya miji hiyo. Vilevile, shughuli za uwindaji na uvuaji samaki zitarejea

Makumbusho, kumbi za sinema, maonesho ya sanaa na baadhi ya shule nazo zitafunguliwa huku idadi ya watu ikizingatiwa

Uhispania imerekodi visa 280,117, wagonjwa 196,958 wamepona na waliofariki ni 27,940

MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 25,000 VYATANGAZWA

Takwimu za Chuo cha John Hopkins zimeonesha kuwa visa vipya 25,294 na vifo 1,263 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita

Hadi kufikia asubuhi ya leo wagonjwa 343,811 wa #COVID19 wamepona nchini humo, huku idadi ya waliofariki ikiwa 96,465 na jumla ya visa ikifikia 1.795,587

Rais Donald Trump amesema bendera ya Marekani itapeperushwa katika majengo yote ya serikali pamoja na makumbusho za taifa kwa siku tatu zijazo kuwaenzi Wamarekani waliopoteza maisha kutokana na #CoronaVirus

MEI 21, 2020
CORONAVIRUS: MAJARIBIO YA DAWA YA HYDROXYCHLOROQUINE KUANZA ULIMWENGUNI

Wafanyakazi wa Afya Uingereza na Thailand wameanza kuhusika kwenye majaribio ya kufahamu kama aina mbili za dawa za kutibu Malaria zitaweza kuzuia COVID19

Dawa hizo zinajumuisha aina ya dawa ya hydroxychloroquine ambayo Rais wa Marekani, Donald Trump alijinadi kuwa anaitumia akiamini ni nzuri

Utafiti unajumuisha zaidi ya Wafanyakazi wa Afya 40,000 wa barani Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, ili kujua kama chloroquine na hydroxychloroquine inaweza kusaidia kupambana na COVID_19

Uhitaji wa hydroxychloroquine umeongezeka zaidi baada ya Rais Trump kuipigia upatu mapema Aprili na wiki hii alijinadi kuitumia licha ya tahadhari kadhaa kutoka kwa Wataalamu wa Afya


BRAZIL: VISA VIPYA ZAIDI YA 19,000 VYAREKODIWA

Brazil imeripoti idadi kubwa zaidi ya maambukizi kuwahi kutokea ndani ya saa 24 ambapo visa 19,951 vimerekodiwa

Wizara ya Afya imesema visa 19,951 vimerekodiwa jana na idadi ya maambukizi nchini humo imeongezeka na kufikia 293,357

Aidha, vifo 888 vimeripotiwa na jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na COVID19 hadi sasa ni 18,894

Brazil inakuwa nchi ya tatu kwa visa vingi kwa #CoronaVirus nyuma ya Urusi (308,705) na Marekani (1,750,407)


MEI 20, 2020
UHISPANIA: WANANCHI WATAKIWA KUVAA BARAKOA SEHEMU ZA UMMA

Wizara ya Afya imesema wananchi watatakiwa kuvaa barakoa wakiwa sehemu za umma ambazo umbali wa futi 6.5 utakuwa vigumu kuzingatiwa

Wananchi wote kuanzia miaka 6 wametakiwa kuzingatia agizo hilo, watu wenye matatizo ya pumu na wale walio na ulemavu unaozuia uvaaji barakoa hawatohusishwa

Barakoa zote zinaruhusiwa ikiwa zinaziba pua na mdomo lakini Wizara imeshauri wananchi kutumia barakoa zilizothibitishwa kitaalamu

Uhispania imerekodi jumla ya visa 278,803, vifo 27,778 na wagonjwa waliopona ni 196,958

BRAZIL: VIFO ZAIDI YA 1,000 VYAREKODIWA KWA SIKU MOJA

Wizara ya Afya imesema vifo 1,179 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa nchini Brazil tangu kuanza kwa mlipuko wa Corona

Nchi hiyo ina visa 271,885 na vifo 17,983 hadi sasa, huku jumla ya wagonjwa waliopna Virusi hivyo ikiwa 106,794. Brazil imerekodi visa vingi zaidi kuliko Uingereza (248,818), Italia (226,699) na Ufaransa (180,812)

Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro amekosolewa kwa namna anayokabiliana na janga la COVID19. Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anafikiria kuzuia safari za Brazil

Rais Trump amesema ni kwasababu hataki watu kuingia nchini humo na kuambukiza Wamarekani. Amesema Brazil inapitia wakati mgumu na wanaisaidia na mashine za upumuaji

MEI 19, 2020
UJERUMANI: WATUMISHI WA AFYA ZAIDI YA 20,000 WAPATA COVID19

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini humo kimesema zaidi ya watumishi wa afya 20,400 wameambukizwa CoronaVirus tangu kuanza kwa mlipuko huo

Kwa mujibu wa Taasisi ya Robert Koch, takriban watumishi 19,000 wamepona na 61 wamefariki dunia. Visa vya watumishi vinakadiriwa kuwa 11% ya maambukizi yote ya Ujerumani

Nchi hiyo imerekodi visa 177,620 na vifo 8,150 huku wagonjwa waliopona wakiwa 155,700

MAREKANI: WATU ZAIDI YA 93,000 WAFARIKI DUNIA KWA CORONAVIRUS

Nchi ya Marekani imerekodi jumla ya vifo 93,088 hadi kufikia sasa, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yeyote duniani

Aidha visa 1,721,133 vya COVID19 vimeripotiwa mpaka asubuhi ya leo na wagonjwa wapatao 322,939 wakiwa wamepona

Pamoja na Marekani, nchi nyingine zenye idadi kubwa ya maambukizi ni Urusi (290,678), Uhispania (278,188), Brazil (255,368) na Uingereza (246,406)

Ulimwenguni kote, Virusi vya Corona vimeathiri watu takriban 5,064,492, wagonjwa waliopona ni 1,872,984 na vifo vilivyoripotiwa ni 321,338

MEI 18, 2020
MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 18,000 VYAREKODIWA

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo cha John Hopkins, takriban visa vipya 18,873 na vifo 808 vimerekodiwa jana, Mei 17 2020

Hivi sasa Marekani ina jumla ya visa 1,674,644, wagonjwa waliopona ni 313,809 huku waliofariki dunia wakiwa 92,639

Bado Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi na mlipuko wa COVID19. Mataifa mengine yenye idadi kubwa ya maambukizi ni pamoja na Urusi, Uhispania, Uingereza na Brazil

Ulimwenguni kote, visa viliyorekodiwa ni 4,743,780, waliopona ni 1,698,902 na waliopoteza maisha ni 314,785

MEI 14, 2020
UGANDA: WAGONJWA 13 WAONGEZEKA, VISA VYAFIKIA 139


Wagonjwa hao wapya ni madereva wa malori waliothibitika baada ya sampuli 1,741 za madereva wa malori kupimwa #COVID19 jana Mei 13, 2020

Kati ya Wagonjwa hao wapya, Waganda ni 7, Wakenya ni 5 na mmoja ni raia wa Eritrea ambao wanaelezwa kuingia Uganda wakitokea Tanzania, Sudan Kusini na Kenya kupitia mipaka ya Mutukula, Elegu na Malaba

Aidha, Wizara ya Afya imeeleza kuwa jumla ya sampuli zilizopimwa jana ni 2,104 ambapo sampuli 363 zilikuwa za Wananchi katika jamii mbalimbali nchini humo na zote zilikutwa hazina maambukizi

Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki waliokutana walikubaliana kuwa madereva wa malori watakuwa wakipimwa mara mbili, watapimwa nchi watokako na wataondoka ikiwa wako salama na pia watapimwa nchi wanakoenda

MEI 13, 2020
CORONAVIRUS: URUSI YAREKODI VISA ZAIDI YA 10,000 KWA SIKU YA 11 MFULULIZO


Urusi imeripoti Wagonjwa wapya 10,028 leo Mei 13 na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 242,271. Watu 96 wamefariki usiku wa kuamkia leo na kufanya idadi ya vifo kufikia 2,212

#Urusi inaipita Uingereza yenye visa 226,463 na kuwa nchi ya tatu kwa wingi wa visa nyuma ya Marekani yenye visa 1,490,915 na Uhispania yenye visa 269,520

Aidha, nchi hiyo imesitisha matumizi ya baadhi ya mashine za kusaidia kupumua (Ventilator) zinazotengenezwa nchini humo baada ya mashine mbili za aina hiyo kuwaka moto hospitalini

Aina hiyo ya mashine (Aventa-M) zilikuwa zinatumika katika hospitali ya St. Petersburg ambapo watu watano walifariki kutokana na moto huo, na pia zilikuwa zinatumika katika hospitali ya Moscow ambapo mtu mmoja alifariki

UGANDA: MADEREVA WANNE WA MALORI WAKUTWA NA #COVID19. YUPO MTANZANIA MMOJA

Wizara ya Afya nchini humo imesema Madereva wanne wa malori wamethibitishwa kuwa na #COVID19 na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 126

Wawili kati ya Wagonjwa wapya ni Waganda huku wengine wakiwa ni raia wa Kenya na Tanzania. Waganda na Mkenya wanaaminika kuingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu na Mtanzania alipimwa katika mpaka wa Mutukula

Wamegundulika baada ya sampuli 1,478 za madereva wa malori kupimwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi Uganda. Hadi sasa sampuli zaidi ya 10,000 za madereva wa malori zimepimwa

Upatikanaji wa madereva wa malori wenye #COVID19 imezuia hofu kati ya Waganda wengi wakiogopa madereva hao watasababisha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo

CORONAVIRUS: BRAZIL YAREKODI VIFO 881 NDANI YA SAA 24

Wizara ya Afya imethibitisha jumla ya vifo 12,400 kutokana na #COVID19 huku idadi ya visa ikifika 178,214 na kuipita Ujerumani yenye visa 173,273 huku ikiwa inaikaribia Ufaransa yenye visa 178,228

Baadhi ya nchi za Ulaya zinaanza kupunguza masharti ya zuio la kutotoka ndani, lakini mlipuko wa ugonjwa huo unazidi kuongezeka #Brazil ambapo Rais Jair Bolsonaro amewakosoa Magavana kwa kutoa amri ya watu kujitenga

Wiki hii Rais Bolsonaro aliongeza mzozo baina yake na Magavana wa Majimbo baada ya kuainisha biashara kama Sehemu za Mazoezi (gyms) na saluni ni huduma muhimu hivyo zisizuiliwe

Rais huyo amesema Magavana wasiokubaliana naye katika hilo wanaweza kwenda Mahakamani huku akiwatishia kuwa atachukua hatua za kisheria kwa wale wasiofuata maagizo yake

Hata hivyo, takriban Magavana 10 wamesema hawatafuata agizo hilo. Gavana wa Rio de Janeiro, Wilson Witzel amesema "Bolsonaro anatembea kuelekea bondeni na anataka kutuchukua sisi wote pamoja naye"

MEI 11, 2020
MAREKANI YARIPOTI VIFO ZAIDI YA 80,000. UHISPANIA YAREKODI VIFO VICHACHE


Marekani imerekodi jumla ya vifo 80,807 vya #COVID19 huku ikiwa na jumla ya visa 1,387,047 kutoka katika Majimbo yote 50 na sehemu zilizochini ya nchi hiyo

Taifa hilo ambalo kwa sasa ndilo linaongoza kwa idadi ya vifo na watu walioathirika na virusi hivyo limerekodi jumla ya Wagonjwa 234,916 waliopona hadi kufikia sasa

Aidha, Uhispania imerekodi vifo vipya 123 na kwa mujibu wa Wizara ya Afya idadi hiyo ya vifo ni ndogo kutokea kwa ndani ya wiki 7. Jumla ya Vifo imefikia 26,774

Idadi ya visa nchini humo imeongezeka kutoka 224,390 kwa jana, Jumapili hadi visa 268,143 kwa siku ya leo Mei 11, 2020 huku idadi ya Wagonjwa waliopona ikifikia 177,846

Huko Uturuki, maduka, saluni za aina zote zimeruhusiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa takriban miezi miwili huku nchi hiyo ikihimiza masuala ya usafi zaidi

Hadi kufikia leo, nchi hiyo imerekodi jumla ya visa 138,657, vifo 3,786 huku kukiwa na zaidi ya Wagonjwa 92,691 waliopona ugonjwa huo

URUSI YAREKODI VISA VIPYA 11,656. YAWA YA TATU KWA VISA VINGI ULIMWENGUNI

Urusi imeripoti visa vipya 11,656 leo, na kufanya nchini hiyo kuwa na jumla ya visa 221,344 na kuwa ya tatu Ulimwenguni kwa visa vingi nyuma ya Marekani na Uhispania

Mji Mkuu wa nchini hiyo, Moscow umeathirika zaidi ukiwa umeripoti vifo 658 vya COVID19 kwa mwezi uliopita huku jumla ya vifo 2,009 vikiwa vimerekodiwa nchini humo

Baadhi ya wakosoaji na wataalam wamesema kiwango cha chini cha vifo cha nchini humo kinaficha idadi ya kweli ya vifo vya #COVID19 vinavyotokea

Pamoja na hayo, Urusi (#Russia) imeripoti kuwa jumla ya Wagonjwa 39,801 walipona. Marekani imeripoti visa 1,387,047 huku Uhispania ikiwa na visa 264,663

MEI 10,2020
VISA ZAIDI YA MILIONI NNE VYAREKODIWA DUNIANI

Visa 4,120,788 vya COVID19 vimeripotiwa ulimwenguni huku wagonjwa waliopona wakiwa 1,388,920 na jumla ya vifo ikiwa 280,144

Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi ikiripoti maambukizi 1,369,245 na vifo 80,068 huku waliopona wakifikia 217,636

Mataifa mengine ni Uhispania (262,783), Italia (218,268), Uingereza (215,260) na Urusi (198,676)

Barani Afrika, taifa la Afrika Kusini limerekodi visa 9,440, Misri (8,964), Morocco (5,911), Ghana (4,263) na Nigeria (4,151)

MEI 09, 2020
BRAZIL: VISA ZAIDI YA 10,000 VYA #COVID19 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona imefikia 9,897 huku kukiwa na kesi mpya 751, za vifo nchini Brazil

Wizara ya afya imeeleza kuwa idadi ya walioambukizwa imepanda zaidi hadi kufikia 145,328 huku kukiwa na zaidi ya maambukizi 10,000 ndani ya masaa 24 zilizopita

Brazil inakuwa ni kati ya nchi zilizoathirika zaidi Latin America

MEI 07, 2020
PAKISTAN: WIZARA YA AFYA YATANGAZA VISA VIPYA ZAIDI YA 1,500


Wizara ya Afya ya Pakistan imetangaza visa vipya 1,523 vya COVID19, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa ndani ya saa 24. Nchi hiyo ina visa 24,073 hadi sasa na vifo vimefikia 564 baada ya watu 38 kufariki dunia

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uendeshaji wa Kitaifa (NCOC) maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipuko wa Corona ni Punjab, Khyber Pakhtunkhwa na Balochistan. Idadi ya wagonjwa waliopona ni 6,464

Aidha, Kituo hicho kimeshauri masharti yaliyowekwa ili kudhibiti maambukizi ya CoronaVirus kulegezwa na huduma za usafiri kurejea nchi nzima kuanzia Mei 09 mwaka huu. Pia, kimejadili kuhusu kufungua biashara kabla ya sikukuu ya Eid

MAREKANI: VISA VIPYA ZAIDI YA 24,000 VYAREKODIWA

Kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha John Hopkins, Marekani imerekodi visa vipya 24,252 vya COVID19 na watu wapatao 2,367 wamefariki dunia kwa siku ya Jumatano pekee. Marekani ina jumla ya maambukizi 1,228,603 na vifo 73,431 hadi kufikia sasa

Marekani imerekodi visa na vifo vingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani lakini majimbo mbalimbali ikiwemo Colorado Florida na Georgia yamelegeza baadhi ya masharti licha ya Wataalamu wa Afya kuonya inaweza kusababisha visa kuongezeka

Aidha, imeripotiwa kuwa Mwanaume wa miaka 57 kutoka nchini El Salvador amekuwa mtu wa kwanza kufariki dunia kutokana na CoronaVirus akiwa mikononi mwa Uhamiaji (ICE). Alipata maambukizi kwenye kituo kilichopo San Diego, California na kupelekwa Hospitali ambapo alifariki

MEI 06, 2020
URUSI YAREKODI VISA VIPYA ZAIDI YA 10,000 KWA SIKU YA NNE

Ndani ya saa 24 zilizopita, Urusi imerekodi visa vipya 10,559 vya COVID19. Hii inakuwa siku ya nne mfululizo kwa taifa hilo kuwa na visa zaidi ya 10,000 kwa siku moja

Licha ya ongezeko kubwa la wagonjwa, Urusi imesema idadi ya wanaopoteza maisha imekuwa ndogo kwasababu mlipuko wa Corona Virus ulichelewa kuingia nchini humo tofauti na sehemu nyingine na Mamlaka zilipata muda wa kujiandaa

Urusi ina jumla ya visa 165,929 na waliofariki dunia ni watu 1,537. Rais Vladimir Putin ameagiza amri wa wananchi kutotoka nje kuendelea kutekelezwa mpaka Jumatatu

UJERUMANI: SHULE, MADUKA KUFUNGULIWA MWEZI HUU

Katika jitihada za hali kurejea kama awali, Ujerumani itafungua Shule na maduka yaliyokuwa yamefungwa ili kudhibiti maambukizi za CoronaVirus nchini humo

Taarifa ya makubaliano baina ya Kansela Angela Merkel na Wakuu wa Mikoa imesema Shule zinatakiwa kuendelea kufundisha wanafunzi huku tahadhari za usafi na ukaribu zikizingatiwa

Awali, Wanafunzi waliokuwa wakikaribia kufanya mitihani ndio waliruhusiwa kurudi Shuleni lakini kuanzia wiki ijayo, Shule za awali na msingi zitafunguliwa

Kuhusu maduka, wamesema yanaweza kufunguliwa ila yametakiwa kuzingatia usafi, kusimamia mahali watu wanapoingia na kuepusha foleni ndefu ya huduma

Aidha, mikusanyiko ya michezo, matukio ya utamaduni na matamasha bado imepigwa marufuku. Kuna uwezekano kuwa haitaruhusiwa mpaka Agosti 31 mwaka huu

Hata hivyo, Ligi Kuu soka nchini humo, Bundesliga iliyokuwa inatarajiwa kuanza Mei 15 haitaanza baada ya Kansela kusema Wachezaji wote wa Ligi hiyo lazima wakae Karantini kwa wiki mbili kabla Ligi kuendelea

Ujerumani imerekodi visa 164,807, vifo 6,996 na Waliopona 137,400 hadi kufikia leo

MEI 05, 2020
URUSI: VISA ZAIDI YA 10,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24


Urusi imerekodi visa vipya 10,102 vya COVID19 vilivyotokea ndani ya saa 24 zilizopita na hivi sasa maambukizi yamefikia 155,370. Hii inakuwa siku ya tatu mfululizo kwa nchi hiyo kuwa na visa 10,000 kwa siku

Mji Mkuu wa Moscow umetajwa kuwa kitovu cha mlipuko huo ikiwa na takriban nusu vya visa vyote vilivyorekodiwa. Meya Sergei Sobyanin ametahadharisha uwepo na maambukizi zaidi na kuwataka wananchi kuheshimu taratibu zilizowekwa

Urusi inakuwa nchi ya saba duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi nyuma ya Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Uhispania na Marekani. Licha ya ongezeko kubwa la maambukizi, Urusi imerekodi vifo vichache ikilinganishwa na mataifa mengine. Waliofariki dunia ni watu 1,451

MEI 04, 2020
JAPAN: WAZIRI MKUU AONGEZA MUDA WA HALI YA DHARURA MPAKA MEI 31


Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema ni mapema sana kulegeza masharti yaliyowekwa ili kudhibiti mlipuko wa CoronaVirus, hivyo Serikali imesogeza mbele hali ya dharura hadi Mei 31, 2020

Awali, Abe alitangaza hali ya dharura kwa mwezi mmoja kuanzia Aprili 07 mwaka huu katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Tokyo pamoja na mikoa mingine sita lakini baadae hali hiyo ilitangazwa kwa nchi nzima ya Japan

Hadi kufikia leo, Japan imerekodi visa vya 14,877 COVID19 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikiwa 3,981 na waliofariki dunia ni 487

ITALIA YAANZA KULEGEZA MASHARTI

Nchi ya Italia ambayo imekuwa karantini kwa takribani miezi miwili imeanza kulegeza masharti yaliyowekwa ili kuthibiti maambukizi ya COVID19 ambapo kuanzia leo, Wananchi wataruhusiwa kutembea ndani ya miji waliopo

Inakadiriwa kuwa watu wapatao Milioni 4 watarudi kazini, migahawa itafunguliwa lakini itatoa huduma za kununua na kuondoka (Takeaway) pekee. Baa, Shule, sehemu za kufanya mazoezi (gym) zitaendelea kufungwa na wananchi wote wametakiwa kuvaa barakoa

Aidha, safari za nje ya mikoa hazitaruhusiwa na watu wataruhusiwa ikiwa ni kwa ajili ya kazi, sababu za kiafya na dharura.Masharti ya misiba nayo yamelegezwa na sasa watu 15 wataruhusiwa kuhudhuria. Mikusanyiko ya ibada na harusi bado imepigwa marufuku

Italia imerekodi maambukizi 210,717 hadi kufikia leo. Idadi ya wagonjwa waliopona ni 81,654 na waliofariki dunia ni 28,884

VISA ZAIDI YA MILIONI 3. 5 VYARIPOTIWA DUNIANI

Ugonjwa wa #COVID19 umeathiri takribani watu 3,566,201 duniani kote. Hadi kufikia sasa, vifo 248,285 vimeripotiwa na idadi ya wagonjwa waliopona ni 1,154,023

Marekani imeathirikia zaidi na mlipuko wa CoronaVirus ambapo visa1,188,122 vimethibitishwa na idadi ya waliofariki imefikia 68,598. Mataifa mengine yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa ni Uhispania (247,122), Italia (210,717), Uingereza (186,599) na Ufaransa (168,693)

Rais Donald Trump amesema anaamini kuwa chanjo ya Corona itapatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Pia ameeleza kuwa anatamani kuona shule na vyuo vikifunguliwa mwezi Septemba

Naye Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewashukuru watoa huduma muhimu na kutoa wito kwa Mashirika ya Kisayansi kuendelea kutafuta chanjo ya COVID19. Amesema endapo jaribio lolote likifanikiwa, chanjo inapaswa kupatikana duniani kote

Aidha, kwa bara la Afrika, nchi ya Afrika Kusini imerekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi (6,783) huku ikifuatiwa na Misri (6,465), Morocco (4,903), Algeria (4,474) na Nigeria (2,558)

MEI 03, 2020
CDC: MAFUA YANAUA ILA #COVID19 NI HATARI ZAIDI, HAVIPASWI KUFANANISHWA


Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimetoa sababu za kutofananisha mafua ya kawaida na #COVID19 ili kuweka sawa wanaopinga na kutaka shughuli za kiuchumi ziendelee kwa kuamini mafua ni sawa na #COVID19

Kituo hicho kimesema, Mafua ya kawaida yanaweza kuambukiza kwa wastani watu 1.28 wakati #CoronaVirus huambukiza wastani wa watu 2 hadi 3.Pia, Mafua ya kawaida yana chanjo, #CoronaVirus haina chanjo

Aidha, tafiti za CDC zinaonesha kati ya Oktoba 2019 hadi mwanzoni mwa Aprili 2020 mafua yameua wastani wa watu 331 kwa siku huku #COVID19 kuanzia Februari 6 hadi Aprli 30, ikiwa imeua wastani wa watu 769 kwa siku huko Marekani

Pia, Mafua ya kawaida watu huugua siku moja hadi nne baada ya kupata maambukizi, na huchukua siku mbili kuonesha dalili jambo linaloweza kuwafanya wakae nyumbani mara tu wajihisi wagonjwa lakini #COVID19 huchukua siku 4 hadi 5 kuanza kujionesha na kupevuka kwa dalili huchukua hadi siku 14
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment