Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii.
Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.
Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.
1. Chagua wazo unalolipenda
“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.” Alisema
Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.
Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.
2. Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu
Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.
3. Zingatia swala la fedha
Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.
Soma pia: Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo.
4. Angalia uhitaji wa soko
Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.
5. Ushindani
Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza.
0 Comments:
Post a Comment