MASWALI 10 YANAYO ULIZWA MARA KWA MARA KWENYE INTERVIEW

Kujiandaa kwa interview ni kazi nzito kwa watafuta ajira wengi.

Yaani, unaanzia wapi? Una tazamiaje maswali atakayokuuliza mwajiri?

Unajibuje maswali ya interview?

Wasiwasi wa kuwaza interview insababisha wagombea wengi kuwa na hofu na hivyo kumfanya afanye kosa kubwa kabis, kuongea bila mpangilio.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Kwanza, toa mfano wa kazi uliyofanya na jinsi gani ilikusaidia kutatua tatizo linalo kumba hiyo kampuni hivi sasa. Kwa mfano, “kwenye ofisi yangu ya zamani, nilikuwa na changamoto la _________ kilichokuwaa na matatizo zinazofanana na hii.”

Baada ya hapo, elezea hatua ulizochukua kutatua tatizo hili.

Malizia kuelezea matokeo yake na jinsi gani ulichojifunza kwa kupitia hayo kitasaidia kampuni hiyo na changamoto zake.

Sasa, kwa kuwa unajua namna ya kujibu maswali, ujiandae na maswali yapi?

Zifuatayo ni orodha yetu ya maswali 10 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interview na maana zao:

1. Tupe maelezo mafupi kuhusu wewe

Hapa, mwajiri hataki kujua kuhusu maisha yako binafsi, familia yako au unachopenda kufanya nje ya kazini. Mwajiri anataka umueleze kwa ufupi kuhusu kazi ulizofanya. Ulifikaje hapa na unataka kufika wapi.

Kwa hili, andaa maelezo ya kazi ulizofanya isiyozidi sekunde 30 na jinsi gani kazi hizi zimekuandaa kwa nafasi hii.

Dokezo la ziada: Toa maelezo kwa kumhadithia uliyoyapitia. Usiseme “mwaka 1999 nilienda Chuo Kikuu cha Smith kusoma Masoko. Mwaka 2004 nikapata kazi yangu ya kwanza…”

Badala yake sema:

“Mapenzi yangu na masoko yalianza nilivyokuwa na miaka 12. Kuna tangazo la Coca Cola lililokuwa linaongelea kombe la dunia. Hapo ndipo nilipojua kwamba nataka kutumia maisha yangu kutoa hadithi zinazowaunganisha watu na makampuni, kwa hiyo nikajiunga na Chuo Kikuu cha Smith – yenye moja kati kozi bora ya shahadaya masoko nchini Marekani, na baada ya kumalizi nikapata kazi _______. Baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu pale, nilianza kutamani changamoto mpya ya kikazi. Ndio maana niko hapa leo”

2. Kwa nini tukuajiri?

Kama unataka kubaki kwenye fikra za mwajiri zaidi ya wengine, usiwape orodha ya sifa zako – mwajiri anazijua tayari kupitia CV yako. Badala yake, waambie utawasaidiaje kutatua matatizo na changamoto zao. Kutoa jibu kamilifu hapa, waeleze ni jinsi gani utwasaidia wao badala a jinsi gani watakusaidia wewe.

3. Sifa yako kubwa ni nini?

Hii ni nafasi yako kuelezea sifa ulionayo ambayo unajua ni muhimu kwa kampuni hiyo na nafasi hiyo unayoitaka. Ila, usifanye kosa la kusema “mimi ni hodari kwa kuwasiliana”. Badala yake, toa maelezo kwa kuhadithia.

Kwa mfano:

“Sifa yangu kubwa ni ujuzi wangu kwenye kuwasiliana. Hii ilithibitishwa nilivyobidi kuonyesha maadili ya kampuni ____ kwenye soko jipya. Ilibidi ni fanye utafiti juu ya mahitaji na maadili ya wakazi wa eneo hiyo na kuandaa matangazo ya redio yaliyosisitiza maadili hayo na kuonyesha namna gani kampuni hiyo ilihusiana na maadili hayo. Matokeo yake ni kwamba tuliongeza ______ kwa 27% ndani ya mwaka mmoja. Sababu kuu ya hii ni kwamba tuliweza kuwasilisha ujumbe wetu kwenye mazingira ya pale.”

4. Upungufu wako mkubwa ni nini?

Hapa, waajiri wanataka kuona kama unajijua, kama unaweza kukubali kwamba una mapungufu na zaidi ya hapo, kama uko tayari kuzifanyia kazi.

Kwa hiyo, fikiria pungufu ambalo halina umuhimu mkubwa kwa kazi hiyo alafu ongelea hatua ulizochukua au utakazochukua kujiboresha hapo.

Usiseme kwamba huna pungufu lolote. Kila mtu anapungufu au mapungufu.

5. Kwa nini unataka kufanya kazi hapa?

Hili swali pia halihusu jinsi gani kampuni itakusaidia wewe ila, jinsi gani utakuwa faida kwao.

Utafiti juu ya kampuni utakaokuwa umefanya ulivyokuwa unaandaa CV na barua ya kuomba kazi itakusaidia hapa. Fikiria jinsi gani nafasi hiyo unayotaka itasaidia kampuni na kwa nini una nia ya kufanya kazi hapo.

Waajiri wanatafuta watu wenye hamu ya kufanya kazi kwao na sio kwamba ni mtu anayetafuta ajira tu. Wanatafuta watu wenye shauku na mawazo. Huu ni muda wako wakuonyesha mawazo yako.

Kwa mfano:

“Nina nia ya kufanya kazi nanyi kwa vile nimetambua kwamba soko liko katika mabadiliko na ninataka kuwasaidia kuongezea ufanisi na kukua kwa kampuni. Najua kazi itakuwa ngumu lakini hiyo ndio changamoto ninayoitafuta hivi sasa.”

6. Kwa nini uliacha kazi pale ulipokuwa?

Usimseme vibaya mwajiri wala wafanyakazi wako wa zamani. Badala yake, sema tu kwamba unatafuta “changamoto mpya ya kikazi”, ila eleza zaidi kwa kuwaambia jinsi gani kazi hii itakupa changamoto ulizokosa kwenye kazi uliyoacha.

7. Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa?

Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano,

“Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”

8. Toa mfano ya tatizo ulilokumbwa nayo na ulichofanya kulitatua

Mradi umejiandaa kujibu hii swali, halitakupa shida.

Chaguo mfano unaoonyesha ujuzi muhimu inayohitajika kwa kazi hii.

9. Unatarajia kupata mshaara wa kiasi gani?

Hakikisha unafanya utafiti juu ya viwango vya mishaara kwa nafasi hiyo na kwamba umeshafikiria hili. Ingia na viwango viwili, ya chini iwe unayoweza kukubali na ya juu iwe unayopenda.

Usipojiandaa na ukajaribu kuhisia, unaweza ukaishia kujionea.

10. Una maswali yoyote ya kutuuliza?

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:

  • Maadili ya kampuni
  • Aina ya uongozi
  • Wafanyakazi wenzako
  • Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  • Watakupa jibu baada ya muda gani?

Swali la ziada:

Baada ya miaka 5, unataka uwe umefikia wapi?

Mwajiri atakuuliza hili swali kujua kama utafuta ajira tu kupata mshaara au kama kweli unataka hii kazi kwa sababu umeipenda na inaendana na malengo yako ya kazi. Kwa hiyo, kwa kuwa wengi wetu hatujui kwa uhakika ni wapi tutakapofikia baada miaka 5, jaribu kufikiria hilo.

Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa

Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri, kama chochote maishani. Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu zitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa.

Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment