LIST YA MABILIONEA WA AFRICA MO DEWJI ATAJWA.

Sub-Saharan Africa Has Fourteen Billionaires

Jarida la Forbes limetoa orodha mpya ya mabilionea wa Afrika walioweza kubaki kwenye ubilionea wao na walioweza kuufikia ubilionea hadi Januari 2020.

Kupitia orodha hiyo, raia wa Nigeria, Aliko Dangote ameendelea kukaa kileleni akiwa na utajiri wa $10.3 bilioni, ambazo hata hivyo ni pungufu kwa $2 bilioni za mwaka jana. Chanzo cha kupungua kwa utajiri wa Dangote mwenye umri wa miaka 63 kimetajwa kuwa ni kushuka kwa hisa za biashara yake ya Saruji kwa asilimia 20.

Aliko Dangote

Nafasi ya pili imerudi kwa raia mwingine wa Nigeria, Mike Adenuga mwenye utajiri wa $9.2 bilioni. Tofauti na Dangote, kiwango cha utajiri wa Adenuga kimepanda kutoka $5bilioni za Januari 2018. Bilionea huyu anamiliki kampuni ya Simu ya Globacom, inayoshika nafasi ya tatu nchini Nigeria. Pia, anamiliki kampuni inayofanya biashara ya mafuta pamoja na makampuni mengine makubwa.

Nicky Oppenheimer, raia wa Afrika Kusini ameshika nafasi ya tatu katika orodha ya mwaka huu. Utajiri wake umethaminishwa kuwa ni $7.3 bilioni, ikiwa umeshuka kutoka $7.7 za mwaka jana. Alijipatia utajiri mkubwa baada ya kuuza kampuni ya kuchimba madini ya almasi ya DeBeers mwaka 2012. Aliiuza kampuni hiyo iliyoasisiwa na babu yake kwa $5.1 bilioni alizolipwa taslimu.

Katika orodha hiyo ndefu ambayo imeshuhudia kupungua kwa mabilionea watatu kwa kulinganisha na orodha yam waka jana, Mtanzania pekee, Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ametajwa kwenye nafasi ya 16 akiwa na utajiri wa $1.9 bilioni.

Mo Dewji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya METL ambayo yaliasisiwa na babu yake mwaka 1970, amebakiza dola kadhaa afikishe utajiri wa $2bilioni. Makampuni ya METL yapo katika nchi sita barani Afrika. Mwaka 2016, aliweka ahadi ya kutoa takribani nusu ya utajiri wake kuhakikisha inasaidia jamii.

Katika orodha hiyo pia kuna wanawake wawili tu, Isabel dos Santos ($2.3 bilioni) akishika nafasi ya nane. Isabel ni mtoto wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos. Anamiliki hisa za makampuni kadhaa makubwa nchini Uholanzi ikiwa ni pamoja na kampuni ya Televisheni ya Nos SGPS.

Mwanamke mwingine bilionea ni Folorunsho Alakija ($1.1 bilioni) ambaye ni raia wa Nigeria na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Famfa Oil inayofanya kazi ya kuchimba mafuta nchini humo.


LIST KAMILI

RankNameNet WorthAgeOrigin of Wealth
#1Aliko Dangote$10.1 B63cement, sugar, flour
#2Nassef Sawiris$8 B59construction, chemicals
#3Mike Adenuga$7.7 B67telecom, oil
#3Nicky Oppenheimer$7.7 B74diamonds
#5Johann Rupert$6.5 B69luxury goods
#6Issad Rebrab$4.4 B76food
#7Mohamed Mansour$3.3 B72diversified
#8Abdulsamad Rabiu$3.1 B59cement, sugar
#9Naguib Sawiris$3 B65telecom
#10Patrice Motsepe$2.6 B58mining

#11Koos Bekker$2.5 B67media, investments
#12Yasseen Mansour$2.3 B58diversified
#13Isabel dos Santos$2.2 B47investments
#14Youssef Mansour$1.9 B75diversified
#15Aziz Akhannouch$1.7 B59petroleum, diversified
#16Mohammed Dewji$1.6 B45diversified
#17Othman Benjelloun$1.4 B87banking, insurance
#18Michiel Le Roux$1.3 B71banking
#19Strive Masiyiwa$1.1 B59telecom
#20Folorunsho Alakija$1 B69oil


Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment