Wanadamu jinsi wanavyodili na matatizo yao ndo inawatofautisha masikini na matajiri, Masikini huwa anamtazamo wake na matajiri huwa na mtazamo wake katika kutatua matatizo.
Kuna tofauti nyingi sana kati ya tajiri na masikini jinsi wanavyofikiri na kuwa na mitazamo tofauti. Mitazamo chanya na kufikri kichanya zaidi kwa matajiri kunawafanya wajizidi kuwa juu ukilinganisha na masikini jinsi wanavyofikiria.
Masikini huwa wanaamini kuwa pesa ndio mzizi wa maovu yote lakini matajiri huwa wanaamini kuwa umasikini ndio mzizi wa maovu yote.
Masikini huwa wanaamini kuwa pesa ni ngumu sana kuipata wakati matajiri huwa wanaamini kuwa pesa ni rahisi kuipata kama ukiitega. Masikini huwa wanaamini kuwa kama wakiwa matajiri watapoteza marafiki wao lakini Matajiri huwa wanaamini kuwa na marafiki kutawaongezea mtandao mkubwa zaidi wa kuwa tajiri.
MAWAZO YA MASIKINI AKIWA NA HALI MBAYA YA KIUCHUMI
1. Anaanza kuwatupia lawama wazazi wake.
Masikini ataanza kuwalaumu wazazi wake kwa nini hwajamfungulia biashara, hajamsomesha mara kwa nini wamekua umasikini.
2. Ataanza kulaumu serikali yake
Ataanza kulaumu hawa ni mafisadi wanasababisha tuwe masikini wanajali familia zao tu.
3. Ataanza kulaumu ukoo wake.
Hapa ataanza kulaumu kwa nini Shangazi anampendelea furani, ukoo mzima umenitenga, mara babu mbona hujanipa mtaji.
4. Ataanza kukata tamaa
Hapa ataanza kusema aah sio lazima niwe tajiri, mara utajiri ni kwa ajiri ya watu kadhaa.
5. Anaanza kusema nimipango ya Mungu
Hapa atasema Mungu akipanga kuwa tajiri nitakuwa.
6. Anaanza kufikiri atakuwa amerogwa
7. Ataanza kusema nina bahati mbaya.
Mwisho wa siku tatizo lake la kifedha litakuwa palepale.
MAWAZO YA TAJIRI AKIWA NA HALI MBAYA YA KIUCHUMI
1. Ataanza kufikiri labda matumizi yangu ya pesa ni mabovu.
Hapa atafikiri kubadilisha matumizi yake ya pesa nina nunua vitu ambavyo sivihitaji.
2. Ataanza kufikiri labda chanzo changu cha pesa ndio sababu.
Hapa ataanza kufikiri labda chanzo changu kimoja cha pesa akisaidie labda niongeze vyanzo vingine.
3. Ataanza kufikiri itakuwa hii ni wakati mbaya wa kiuchumi.
Atafikiri huu ni wakati mbaya wa kiuchumi kwahiyo wakati mwingine wakati kama huu inabidi niwe nime weka kihasi fulni cha kunisaidia wakati kama huu.
4.Ataanza kufikiri labda ujuzi wangu haupo vizuri.
Hapa atafikiri labda kuna kitu hakifahamu vizuri na akikifahamu atapiga pesa.
5. Ataanza kufikiri labda ni madeni.
Hapa atafikiri labda kuwa na madeni kunasababisha mimi kudidimia kiuchumi inabidi ni ache kukopa.
6. Ataanza kufikiri labda hana connection ya kutosha, hana marafiki wanao mpa michongo. Hapa ataanza kufikiri njia za kuongeza watu watao mpa connection na ataanza kuwa socil na watu.
7. Ataanza kujifunza kutoka kwa wengine.
Watu ambao wameendelea kuliko mimi wamewezaje kumaintain mpaka leo, ataanza kifanya research labda biashara yake sio nzuri.
Mwisho wasiku anajikuta amejifunza na kusolve mambo mengi.
Mwisho wa siku utakuta tajiri ataendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini.
0 Comments:
Post a Comment