Pia ikumbukwe tu kwamba ili kukamilisha maono yako ni lazima utahitaji watu fulani kwa namna moja au nyingine watakao kufikisha hatua moja mbele. Kama unataka kufanya biashara ya aina fulani ya watu ambao wanaifahamu vyema biashara husika ambao watakusaidia sana kukushika mkono hasa pale unapokuwa unakwama.
Hivyo kila wakati ni muhimu sana kwako kujenga mtandao na watu sahihi ambao watakuwezesha kwa njia moja au nyingine kufikia lengo lako. Ni muhimu kujuana na watu mbalimbali kwa sababu watu wengine wanakijua kile ambacho wewe hukijui hivyo pindi utakapoamua kushikiana na watu hao watakusaidia sana kujua mengi ambayo mwanzo ulikuwa huyajui.
Waswahili husema,, kosea mengine ila usikosee kuoa/ kuolewa. Lakini katika kufanikiwa pia huwa tunasema, kosea mengine ila usikosee kuwa na mahusiano na mtandao wa watu ambao Si sahihi katika mafanikio.
Hivyo wito wangu kwako ni kwamba unapaswa kujifunza kuchagua watu sahihi watakaokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kufanikiwa katika malengo yako.
0 Comments:
Post a Comment