FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU


FAIDA ZA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI
FAIDA ZA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI

FAIDA ZA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI : Leo ningependa kuchambua faida mbalimbali za kuku wa kienyeji. Imezoeleka katika sehemu nyingi kuku hutumika kama kitoweo, hii ni faida moja wapo ya kuku,lakini pia mayai ya kuku wa asili hua na virutubisho kama Vitamin A, Vitamin E, Vitamin D, Vitamin B12, Madini ya zinc, Madini chuma na pia protein ambayo ni muhimu sana katika ujenzi wa mwili.                                           

Kuku hufugwa kibishara ni ajira nzuri kwa mfugaji. Ufugaji wa kuku huitaji mtaji kidogo katika kuanzisha, pia eneo dogo. Mfano unaweza kuanza na mtaji wa kuku 7, matetea watano na majogoo watatu. Kama kuku hawa watapata chakula kilicho bora kuku mmoja huweza kutaga na kutotoa hadi vifaranga 12. 

 
Hivyo kwa matetea watano huweza kufikisha hadi vifaranga 50. Mfugaji akiweza kulea Angalau vifaranga 40  ukijumlisha na wale Saba wa mwanzo ni jumla ya kuku 47, kwa idadi hiyo ya kuku inamaana kutakua na ongezeko kubwa la utotoleshaji. Kwa wafugaji wasio kua na mtaji mkubwa unaweza kuuza kuku hata kumi kwa bei ya kuanzia 20000/= hadi 25000/=  ambapo huweza kupata laki 2 (200,000/=).
 
Fedha hii ikatumika katika kununua chakula na madawa kupambana na magonjwa kwa njia huu mfugaji huweza hata kufikia kuku 1000 hivyo kufanya mfungaji.
 
Kuwa na mtaji wa 20,000,000 kwa wasio na maeneo ya kutosha ,usiogope biashara hii hujiendesha yenyewe ukianza vizuri unaweza kuuza mayai au kiasi fulani cha kuku ,fedha hiyo ikatumika katika kujiendeleza katika biashara hii.
 
kuku huliwa kila siku sehemu mbali mbali kama kwenye migahawa, hotelini na kwa mama ntilie hivyo solo lake in la uhakika.
 
Malighafi za kujengea band la kuku hupatikana kirahisi katika sehemu mbali mbali  hata maeneo ya vijijini. Pia vifaa vyake hupatikana katika maduka ya mifugo na huweza kujengwa vifaa vya asili katika maeneo  yasio na maduka hayo
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment