BIASHARA 10 ZINAZOLIPA ZAIDI

Watu wengi wenye mafanikio zaidi duniani ni wafanyabiashara. Mwanzilishi wa Apple marehemu, Steve Jobs alipoulizwa katika moja kati ya interview na vyombo vya habari, "Ulianza kuendesha kampuni ukiwa na miaka 21, uliwezaje kufanya hivyo ilhali hauna uzoefu na taaluma hiyo", Jobs alisema,"..hakuna mfanyabiashara anayejua jinsi anavyofanya biashara, anafanya kwa sababu anashtukia ameshafanya na jambo la ajabu ni kwamba hufanikiwa..". Ok, simaanishi we nae ukurupuke tu uanze biashara bali ninakuambia tu uache wasiwasi na labda biashara ndiyo nyota yako.

Kama ungependa kuanzisha biashara Afrika Mashariki, iwe Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, hizi ndizo biashara 10 zinazolipa zaidi, ninamaanisha kuwa wafanyabiashara waliofanikiwa ukanda huu, hufanya biashara hizi.

10. Migahawa na Fast food




Angalau kila binadamu anatakiwa kula chakula ili aweze kuishi. Maeneneo makubwa ya miji kama Nairobi, Kampala na Dar es salaam yanakua kwa kasi na hivyo idadi ya watu kuwa kubwa zaidi. Wafanyabiashara wengi wanaofanya biashara hii kiufasaha wanaweza kukua zaidi na kuwa na biashara kubwa sana.



9. Tiba Asili.
Kama ilivyo kwa nchi nyingi Afrika tiba asili zimekuwa zikiaminika kuwa bora zaidi. Hata nchi za wenzetu walioendelea kama China hupenda dawa za asili kwani hazina kemikali. Siyo kila mtu anaweza kufanya biashara hizi. Huhitaji uzoefu na lazima upate idhini ya serikali kama tiba ni salama.

8. Saluni na Urembo.
Siku hizi masuala kama Pedicure, Manicure na masaji yamekuwa mambo yanayotiliwa maanani na jamii za wa Afrika mashariki. Hair dressing na kunyoa ni kama mambo ya lazima kwa mtu yeyote mwenye kuhitaji kuwa mtanashati. Biashara hii inaendelea kuwanufaisha wengi kama ukitoa huduma nzuri na za kipekee.




7. Famasia na Madawa.
Ili kufanya biashara hii utahitaji elimu na uzoefu lakini faida utaipata. Magonjwa hayaishi. Hivyo watu wanaofanya biashara hii ya kuuza madawa na vifaa vya famasia wamekuwa wakipata mapato mazuri na faida kwa ni biashara yenye uhakika wa kuuzika.

6. Vifaa vya ujenzi.
Watu wanajenga kila siku. Vifaa vya ujenzi hununuliwa na kuisha kabisa madukani. Viwanda haviishii kutengeza bidhaa. Nani hapendi ujenzi?


5. Vito vya thamani.
Urembo ni jadi ya waafrika waliojaliwa ubinufu wa mawazi na kuwa wenye muonekano mzuri kwa watu. Zaidi biashara ya vito vya thamani huwavutia pia watu wa mataifa yote duniani. Biashara hii inashika nafasi ya kati (5/10) katika biashara zetu kumi zenye malipo bomba zaidi Afrika mashariki.

4. Vifaa vya uani.
Vifaa kama Toilet paper, diaper za watoto, dawa za choonin na sabuni zimeshika kasi katika soko ukanda huu wa Afrika Mashariki. Vitu kama tissue hutumika mahotelini na katika hafa mbalimbaili kama unahitaji kupiga bao, chukua fursa hii.

3. Pombe na Vilevi. (Tunaomba radhi kwa wasiopendezwa)


Makampuni kama TBL yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kufanya biashara hii. Vilevi vingine kutoka nje ya nchi vimepata umaarufu sana Afrika Mashariki. Sababu kubwa ni kwamba watu wanapenda kuburudika ndio maana ukianzisha biashara ya kuuza vinywaji hivi utafanikiwa.

2. Vifaa vya Elektroniki.
Hii ni moja kati ya biashara kubwa mbili ukanda huu. Tanzania pekee inaongoza kwa watu wengi kumiliki simu za mkononi. Biashara ya vifaa vya elektroniki Afrika Mashariki inalipa kwa kiasi kikubwa sana. Fikiri vifaa kama friji, computer. Mjasiriamali mwenye malengo haswa ataipenda zaidi biashara hii.

1. Vipodozi.
Bila shaka bingwa ndiye huyu. Hii ni biashara yenye mauzo makubwa zaidi Afrika Mashariki. Wanawake wengi hupenda kutumia vipodozi. Jumla ya idadi ya wanawake ni kubwa sana ukilinganisha na idadi ya wanaume Afrika Mashariki. Wanaume pia hununua vipodozi. Kama hauna uhakika ni biashara gani uanzishe, hili ndilo kimbilio lako.


Nimatumaini kuwa umeweza kuziona biashara zinazofanya vizuri zaidi Afrika Mashariki. Ni vizuri unapotaka kufanya biashara ufanye utafiti wa kina juu ya biashara hiyo pia soko linaendaje kwa wakati husika. Usisite ku shea hii na wanajami wenzako hapa mtandaoni!
Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment