JINSI YA KUISHI BILA KUGOMBANA NA MPENZI, MKE AU MWENZI WAKO.






                                                            

Hivi karibuni ugomvi kwenye mahusiano imekuwa kama ni jambo la kawaida. Watu wanagombana kwelikweli. Utakuta mtu haipiti mwezi mmoja bila kugombana na mpenzi wake. Anampenda, hayupo tayari kumpoteza lakini maisha yao kila siku ni ugomvi. Mara nyingi ugomvi unapotokea, ladha ya pendo hupungua.

Inachukua muda kurudi kwenye upendo wa awali mara baada ya wapendanao kugombana. Wahusika wanakuwa wanaukataa ugomvi lakini wapi, baada ya muda unatokea.


“Wakati mwingine unatamani kumuepuka kwa kutokutana naye au kutomsemesha kabisa. Labda unapata furaha ukiwa peke yako kuliko unapo kuwa na Mwenzi wako, inafika mahali mpaka unawaza uachane naye au vipi.”

FANYA HAYA UTAFANIKIWA?

Unapokutana na hali kama hiyo, unapaswa kutulia na kufanya maamuzi sahihi. Usikurupuke. Jiulize ni nini hasa kinachosababisha mgombane? Sema vizuri na moyo wako. Usijipendelee, kama unaona kuna kitu kinachosababisha mgombane na wewe ndio chanzo unapaswa kukishughulikia.

Kama unaona kuna kitu mwenzako anakikosea, tafuta muda ambao mpo kwenye furaha na uzungumze naye kwa lugha rafiki. Muoneshe kwamba haipendezi mnapokuwa mnagombana mara kwa mara. Mueleze kwamba mnapofanya hivyo penzi lenu linapoteza msisimko. Mueleze kwamba ni hatari kuishi katika malumbano maana ni rahisi kujikuta mmeachana. Mfahamishe kwamba kama wote lengo lenu ni moja, kufika mbali kimahusiano kuna sababu gani ya kulumbana kila siku? Mnagombea nini?

MSOME MWENZA WAKO.
Hili ndio somo muhimu katika maisha na mazungumzo yenu. Mueleze kwamba ili muweze kuishi vizuri mnapaswa kuchukuliana upungufu. Nyinyi mmekutana ukubwani. Kila mtu amelelewa katika maadili tofauti. Amekulia katika mazingira tofauti na mkaungana kutengeneza umoja wenu. Mnapaswa kuzungumza lugha moja. Kila mmoja amsome mwenzake kwamba nini anapenda na nini hapendi. Kitu gani huwa kinamuudhi mwenzako? Ukishakijua, epuka kumfanyia maana umeshajua hiyo ndiyo sababu ya nyinyi kugombana.

VUMILIANENENI
Kutokana na kila mtu kuwa na tabia na hulka zake, mnapaswa kuvumilia. Inawezekana kabisa mwenzako akawa na tabia flani ambayo kimsingi si njema lakini unachotakiwa kufanya ni kuibeba. Ishi naye kwa kuirekebisha taratibu. Tumia mbinu za kuzaliwa kumfanya abadilike. Mathalani, unaweza kumchukulia filamu yenye mafunzo kuhusiana na tabia yake na kumuwekea bila kujua kama umemfanyia makusudi. Unaweza pia kumpa majarida mbalimbali au magazeti yenye ujumbe unaohusu tabia yake naye akajifunza.

MFANYE AWE RAFIKI
Kumfanya mpenzi wako awe rafiki yako kutakufanya ujue mpenzi wako anapenda nini na nini hapendi. Hakikisha unakuwa naye karibu, mnazungumza kama marafiki hivyo kukupa mwanya mzuri wa kumuelewa vitu ambavyo huwa havipendi. Unapomweka karibu, anaweza kuwa anakusimulia juu ya mtu flani ambaye amemkwaza labda kwa kumfanyia jambo flani, ni rahisi na wewe kugundua kwamba hapendi kufanyiwa jambo hilo, ukaepukana nalo.


ACHA COMMENT YAKO AU KAMA UNASWALI NITARIJIBU



Share on Google Plus

About Anonymous

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment